Kusadikika
Publisher
Mbiu Press
Language
Swahili

Rent This Book

Expires on August 02, 2025

TSh 2,000/=

Choose Option

BOOK OVERVIEW

Kusadikika ni riwaya fupi inayozungumzia athari za ujinga ,ubinafsi na tamaa mbaya za viongozi katika jamii. Mwandishi ametumia mandhari ya kufikirika yaani angani ilikuifanya hadhira yake isihoji mambo mengi kwani nchi hiyo imekosa mawasiliano ya ana kwa ana na nchi za jirani.

Ujinga ni mbaya sana kwa watu wa kawaida lakini ni maafa makubwa ikiwa ujinga utakuwa ni wa kiongozi hasa aliye wa ngazi ya juu. Katika riwaya ,viongozi wa nchi ya Kusadikika wamepewa mamlaka makubwa kiasi kwamba chochote wakisemacho ni amri.  

Kila jambo katika nchi hii lazima lianzishwe na viongozi ama watu wenye nasaba bora. Jambo hili ni hatari sana hasa ikiwa kiongozi mwenyewe ni mtu aliyejaa chuki na wivu.  Kwa Mazingira haya, raia ambao ni watu wasio na vyeo, walipata shida kubwa sana katika nchi hii.

Karama, mhusika mkuu na raia wa kwanza katika nchi ya kusadikika kupata nafasi ya kujitetea katika nchi hii ametumia kipawa chake cha kujieleza mbele ya baraza na kuonesha udhaifu wa viongozi wa nchi ya Kusadikika walioshindwa kuona manufaa ya utafiti uliofanywa na wajumbe waliotumwa kwenda katika nchi mbalimbali. Awali, kusadikika ilikuwa imetuma wajumbe kwenda pande sita za nchi ya kusadikika ambazo ni kaskazini, kusini, mashariki, magharibi, mbinguni na ardhini. Marejeo na matafiti yaliyofanywa na wavumbuzi hawa yalionekana kuwa ni bure ghali.

Mashitaka ya karama yalikuwa ni kuanzisha elimu ya uanasheria ambayo ililenga kuwaamsha wanakusadikika juu ya uonevu uliokuwa unafanywa na watawala. Jambo hili liliamsha hasira kali ya serikali juu ya mtu huyu aliyeonekana kama msaliti. Ukweli daima utashinda japo waweza kucheleweshwa. Karama anaamua kuusema ukweli. Ukweli ni mchungu na hakika msema kweli hukimbiwa na marafiki zake. Karama haogopi kusema kweli wala hajali yatakayompata.

Ni mambo gani ambayo yaliwapata wajumbe waliotumwa na serikali ya kusadikika kwenda nchi za jirani kutokana na taarifa walizozileta na yapi yalimpata Karama, raia anayetuhumiwa kukaidi amri halali za nchi ya kusadikika? Fuatana na mwandishi wa riwaya hii ili uweze kupata majibu ya maswali hayo pamoja na mengin emengi ya kuvutia.

COMMUNITY REVIEWS

There are no reviews for this book yet

Write a Review