BOOK OVERVIEW
Wapiganaji kumi, wakiwemo watanzania watatu, wanaounda kikosi maalumu cha jeshi la umoja wa mataifa kilichotumwa kulinda amani nchini Sierra Leone, wanashambuliwa na mdunguaji aliyejifich katika msitu waliokuwamo. Sita kati yao wanauwawa, mmoja baada ya mwingine, kwa kudunguliwa na mdunguaji huyo hatari. Ni mtanzania mmoja tu ndiye anayerudi nchini akiwa hai, akirejeshi nyumbani miili ya wapiganaji wawili waliouwawa na mdunguaji huyi huko Sierra Leone. Miaka mitatu baadaye, mpiganaji aliyeshinda vita vingi vya msituni Baddi Gobbos, anajikuta akikabiliana na vita vingine katikati ya jiji la Dar pale anapojiuta akiwindwa na wauaji asiowajua. Je, mdunguaji wa Sierra Leone kaingia Tanzania? Wakati huo huo Badi Gobbos anajikuta akiwa mateka aliyeshiindwa, katika vita ngumu kuliko vyote alivyowahi kukabiliana navyo maishani mwake....vita vya mapenzi