Hisia Zangu
Publisher
Uwaridi
Language
Swahili

Rent This Book

Expires on August 02, 2025

TSh 1,600/=

Choose Option

BOOK OVERVIEW

ALIKUWA msichana mbichi kabisa. Mrembo asiyefananishwa na mwingine katika chuo alichokuwa akisoma - Chuo Kikuu cha Dar es Salaam - Mlimani jijini Dar es Saalam. Pamoja na urembo wake, Lilian alikuwa mwenye bidii sana na masomo. Hata aina ya rafiki zake walikuwa ni wale wenye bidii ya masomo kama yeye. Ni kama walichaguana, wote majina yao yakianziwa na herufi L - Lilian, Leyla, Linna na Lucy. Tofauti yao ilikuwa kwenye tabia tu, lakini kwenye masomo walikuwa wanafanana. Pamoja na kulelewa katika maadili, akiwa bado ameutunza usichana wake, Lilian anakutana na mtu wa ajabu katika maisha yake chuoni hapo. Edward au Edo, kijana mtanashati lakini mwenye historia ya kuwa na msururu wa wasichana, anauteka moyo wake. Anaishiwa uamuzi wa moyo na kuamua kuingia kwenye ulimwengu wa mapenzi na Edo, huku sharti likiwa moja tu; wangekutana kimwili baada ya kufunga ndoa. Edo anaamua kuachana na tabia za hovyo, baada ya kujiridhisha kuwa Lilian ndiye mwanamke wa maisha yake. Anaanza maisha mapya akiwa mwenye nidhamu kwenye uhusiano. Edo anahitimu masomo yake na kumuacha Lilian chuoni hapo. Baadaye Edo anakwenda nchini Malaysia kuendelea na masomo yake katika ngazi ya Shahada ya Uzamili. Huku nyuma Lilian anakutana na Pam ambaye anabadilisha kabisa historia ya maisha yake. Ilikuwa usiku mmoja tu, saa chache ambazo zilisababisha maisha yake yawe mapya kwa kila kitu! Pam, baba mtu mzima mwenye fedha zake anakuwa sababu ya kuharibu masomo yake, uchumba wake, ahadi zake na maisha yake kwa jumla. Lakini pamoja na yote hayo, Edo anafanya uamuzi ambao unamchanganya zaidi Lilian na kushindwa kuamini kama angefi kia uamuzi huo. Je, nini kimo katika kisa hiki? JOSEPH SHALUWA anakuonyesha uwezo wake wa kucheza na fasishi simulizi. Fuatilia ndani...

COMMUNITY REVIEWS

There are no reviews for this book yet

Write a Review