Watoto wa Maman’tilie
Publisher
Lantern-E-Books
Language
Swahili

Rent This Book

Expires on August 01, 2025

TSh 2,000/=

Choose Option

BOOK OVERVIEW

Katika riwaya hii ya Watoto wa Maman’tilie, mwandishi anathibitisha kuwa mama ni mtu wa muhimu sana. Riwaya inasimulia na kushadidia kuwa Maman’tilie ni nguzo na dereva wa familia yake yenye wasafiri watatu: Lomolomo mumewe, mzee asiye na ajira, bali mlevi wa pombe ya gongo; na watoto wao wawili, Zita na Peter, ambao kufumba na kufumbua wanafukuzwa shule kwani wazazi wameshindwa kuwalipia karo. Katika hali hii ngumu, mtoto Peter, kwanza anakuwa chokoraa, akiokota na kula vyakula vya jalalani; na baadaye anajiunga na genge la wauza dawa za kulevya.

Uovu na uvunjifu wa sheria unasababisha Peter kuishia jela. Lomolomo naye anaishia kufa kwa kunywa pombe zenye sumu. Pia, Zita anakufa kutokana na kung’atwa na mbwa mwenye kichaa.


Riwaya ya Watoto wa Maman’tilie ina mafunzo muhimu sambamba na kutoa burudani kwa wanafunzi na jamii yote kwa jumla. Mwandishi wa riwaya hii, Emmanuel Mbogo, ni mtunzi mwenye tajiriba ya miaka mingi katika uandishi wa riwaya, tamthilia na hadithi fupi. Baadhi ya vitabu vyake, zaidi ya kumi na tano, vimeorodheshwa katika ukurasa wa mwisho wa kitabu hiki.


Mwandishi amewahi kufundisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Moi, Chuo Kikuu cha Maseno, Chuo Kikuu cha Kenyatta, Chuo Kikuu cha Kigali na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

COMMUNITY REVIEWS

There are no reviews for this book yet

Write a Review