
BOOK OVERVIEW
Habari ya kuuawa kwa mtafiti Grayson Mochiwa haikuwa na sababu yoyote ya kumshitua mrembo Zay, mpaka pale anapogundua kuwa kutoweka katika azingira ya kutatanisha kwa rafiki yake kipenzi sio tu hakukuwa kwa bahati mbaya bali pia kulihusisha moja kwa moja kibaya cha mtafiti Grayson Mochiwa.
Anajikuta kwenye mtnziko mkubwa pale anapobaini kuwa matukio yale awili yalikwuwa nu sehemu mkakati mkubwa wenye usaliti wa kutisha kwa taifa.
Je aweke matumaini yake kwenye vyombo vya dola huku muda wa kumsaka rafikiye ukizidi kumtupa mkono? Au ajitose mwenyewe kumtafuta rafikiye huku akiyaweka rehani maisha yake?
Ni mpaka pale mazingira yanapomkutanisha na askari wawili asiowatarajia, ndipo anaposhuhudia jiji la likifukuta kwa mikabala mizito, mauaji ya kutisha, usaliti usiosemeka na hekaheka zainazoliingiza taifa kwenye machafuko makubwa.
Kwenye MTAFITI, HUSSEIN TUWA anakukutanisha tena -kwa ufupi sana- na John Vata na Tigfa Mumba, lakini zaidi anakukutanisha na inspekta Haroub Kwakwa (unamkumbuka?) katika ubora wake