
BOOK OVERVIEW
Tamthilia hii inamhusu Bibi Titi Mohamed, mwanamke aliyekuwa mstari wa mbele katika harakati za kudai uhuru wa Tanganyika. Kama mwanachama wa TANU na kiongozi wa Umoja wa Wanawake, Titi alizunguka nchi nzima na hata kwenda nchi jirani kuhamasisha wanawake na Waafrika kwa ujumla kuamka na kudai uhuru wao toka kwa mkoloni bila woga. Wakati wanaume wengi wakiogopa kuchukua kadi za TANU wakihofia "kupoteza kitumbua chao" , kama anavyosema Titi, yeye na wanawake wengine wa Tanganyika waliongoza harakati za kuelimisha na kuhamasisha wananchi wa Tanganyika kuamka na kusaka Uhuru.
Hata hivyo, ujasiri na jitihada za Titi zilimwingiza katika changamoto nyingi za kifamilia. Kutokana na muda mwingi alioutumia kuzunguka kutetea uhuru wa Tanganyika, hatimaye mumewe, Boi, alimwacha na kuamua kuoa mwanamke mwingine.
Tamthilia hii mbali na kuwa na historia muhimu, itakufundisha mengi kuhusu mwanamke huyu mwanamapinduzi na hali ilivyokuwa wakati wa harakati za kusaka uhuru wa Tanganyika. Pia, tamthiliya hii inapatikana kwa njia ya sauti kama mchezo wa kuigiza ikiwa na vionjo vya nyimbo za ukombozi, hotuba na majadiliano kadha wa kadha kati ya Titi, Nyerere na viongozi wengine wa TANU.