Mkimbizi
Publisher
Uwaridi
Language
Swahili

Rent This Book

Expires on August 01, 2025

TSh 4,000/=

Choose Option

BOOK OVERVIEW

Mwanadada Tigga Mumba anaingia kwenye msukosuko mkubwa maishani, pale anaposhuhudia mauaji ya kutisha akiwa msituni akishiriki utafiti wa mambo ya kale. Maisha yanambadilikia pale anapojikuta akishutumiwa kuwa ni yeye ndiye aliyefanya mauaji yale bila kujitambua, kutokana na maradhi ya akili. Paramond Schizophremia!

Kabla hajajua namna ya kuondokana na shutuma zile, anajikuta akiwindwa kwa chambo na ndoano na wauaji hatari hatari wenye hila lukuki, wakiongozwa na muuaji hatari barani Afrika, The Virus; huku jeshi la polisi nalo likimsaka kwa udi na uvumba kuhusiana na mauaji yale, likiongozwa na mpelelezi mahari asiyetetereka, Kamishna Msaidizi John Vata. 

Mambo yanamzuidia ugumu kiasi cha kuutilia mashaka utimamu wa akili yake pale hata watu wake wa karibu wanapomuaminisha kuwa ni kweli amekumbwa na uginjwa wa akiliuliomsukuma kufanya mauaji yale. 

Lakini Tigga anaamini kuwa ana siri kubwa na ya hatari, ambayo wote hawaijui - na ile aendelee kuwa hai na hatimaye aibainishe siri hiyo, analazimika kuishi kwa kukimbia huku na huko akichengana na wauaji hatari, askari waovu, marafiki wa mashaka, huku akikabiliana na mitegi ya kikachero.  

ankkuwa mkimbizi ndani ya nchi yake. Anayekimbia kwa woga na hofu, huku mahala pekee anapokuwa salama ni peke yake na mtu pekee anayejihisi salama kuwa naye ni yeye mwenyewe.

2 COMMUNITY REVIEWS
Hussein Tuwa

Kisa kinatembea na msomaji. Si rahisi kuacha kuendelea kukisoma pindi ukikianza.Namna mwanadada Tigga Mumba anavyawachenga majambazi wabobevu ni hamasa na burudani kubwa. The Virus alinikosha sana, japo ni adui. John Vata moto wa kuotea mbali! A must-read!

  • April 14, 2023  ·  0 found this review useful

Haika Mwitula

Please add book overview

  • July 19, 2022  ·  0 found this review useful

Write a Review