BOOK OVERVIEW
BRIAN anaingia kwenye uhusiano na binti mrembo, mwenye mchanganyiko wa asili ya mataifa tofauti Naima Abdulaziz, kwa kazi maalumu. Ni maelekezo kutoka genge la uhalifu lililokuwa chini ya Mbwira Mwijenga. Naima aliishi Mbezi – Magari Saba, nje kidogo ya Jiji ya Dar es Salaam, ambapo alikuwa akiishi huku akisoma katika Chuo Kikuu cha St. Joseph, kilichopo Luguruni – jirani na makazi yake, chuo ambacho Brian naye alikuwa akisoma hapo. Brian ananogewa na penzi la Naima, mwisho anahiyari kuisaliti kazi yake na kumweleza ukweli wote Naima ili kumnasua kwenye kadhia hiyo. Jambo hilo linaanzisha safari yenye visa vya kusisimua vyenye mchanyato wa siasa, uhalifu, mapenzi na upelelezi. Ni hadithi itakayokuacha na burudani, mafunzo na taharuki ya aina yake. ENDELEA NDANI..