BOOK OVERVIEW
Alipokutana naye mara ya kwanza, alijua amepata mwanamke bora, ambaye angemtuliza maruhani yake akiwa mbali na nyumbani kwake, Mwanza! Mwanamke huyo mzuri kwa kila kitu. Macho mazuri. Sura nzuri. Umbo namba nane, tabasamu tamu na kila kitu kizuri! Haishi hamu kuangaliwa, mwanaume yeyote aliyekamilika lazima akikutana naye achanganyikiwe. Ndivyo ilivyokuwa kwa Bruno ambaye naye alichanganyikiwa na kila kilicho kizuri kwa mwanamke huyu mrembo, Tunu. Kumbe alikuwa anajidanganya. Akaamini ameingia kwenye kiota cha huba, kumbe alikuwa ameingia kwenye tanuru la moto! Tena moto mkali uliosababisha alie kila siku. Asubuhi alie. Mchana alie. Usiku alie. Macho yake yakawa yanadondosha matone ya machozi yanayofanana na damu! Tunu akawa mwiba kwake! Akamsababishia fumanizi, ambalo lilizaa ulemavu unaomtesa. Analia kitandani, akiwa hana msaada wowote. Hakika, hawezi kuisahau Tanga! Ilikuwaje? Hapa Joseph Shaluwa anadhihirisha wazi kuwa amekirimiwa kipawa cha kuandika na siyo kwamba alibahatisha alipotoa kitabu cha SIKUJUA UNGEUTESA MOYO WANGU kilichovunja rekodi ya mauzo nchini Tanzania. Hebu sasa fungua ndani usafi ri naye katika tungo hii kali. Endelea...