BOOK OVERVIEW
Kalabweli alitarajia kuwa angewatunza wazazi wake, dada na wadogo zake kwani alifanikiwa sana katika biashara, akashamiri, akapendwa, akaijua pesa….. Ila ndoto yake haitimii bali inabaki kuwa ndoto. Kisiki Kikavu kinatufunilia maisha ya Kalakweli ambayo yamebeba hsitoria ya UKIMWI huko mkoani Kagera. Historia iliyoanzia katika umaskini uliofuatia vita vya Iddi Amini, hali iliyozaa biashara ya magendo na maisha ya starehe iliyokithiri. UKIMWI ukabisha hodi ukapatiwa majina; Juliana, Silimu, Ninja,…… Kisiki Kikavu kinaweka wazi udhaifu wetu katika kukabili changamoto za maisha. Jinsi unavyozidi kusoma Kisiki Kikavu ndivyo unavyoona kwamba historia, siasa, mila na uchumi vimeshikamana katika kuibua na kutandawaza janga la UKIMWI, na hapo unagundua ukavu wa fikra za mwanadamu. Hii ni riwaya ya aina yake inayochambua taathira za VVU, uelewa wa watu, ukubalifu wao na jinsi tabia zinavyobadilika kwa wakati, mahali na kwa rika. Ni riwaya ninayopendekeza isomwe na kila mmoja anayetaka kujua kwa undani changamoto inayotukabili kuhusu UKIMWI.