
BOOK OVERVIEW
Fungate ya Uhuru ni diwani ya mashairi yanayofichua madhila wafanyiwayo wanyonge na baadhi ya wakubwa, hasa viongozi wanyonyao jasho la wananchi na kujineemesha migongoni mwa wakulima na wafanyakazi. Mashairi haya yanaonesha hasira aliyonayo mwandishi kwani “wakubwa” hawa wanaendelea kujistarehesha huku wakulima na wafanyakazi, ambao ndiyo wajenga nchi, wakiendelea kudidimia katika lindi la dhiki. Hakika, mashairi haya yatamfanya msomaji atafakari uelekeo wa nchi yetu na hapohapo kumchokoza atafute ufumbuzi wa “uyabisi” huu!
Kitabu hiki ni tunu kwa wote wapendao ushairi bora na wenyekupenda kutathmini mwelekeo wa jamii zetu. Vilevile wanafunzi wa fasihi ya Kiswahili shuleni na vyuoni watanufaika na sanaa ya mwandishi katika ushairi huu yenye vionjo maridhawa.