Utubora Mkulima
Publisher
Mbiu Press
Language
Swahili

Rent This Book

Expires on August 01, 2025

TSh 3,000/=

Choose Option

BOOK OVERVIEW

Hii ni riwaya inayozungumzia maisha ya kijana aitwaye Utubora. Kama jina lake lilivyo, kijana huyu anajipambanua kuwa ni mtu jasiri, imara, mvumilivu, mwaminifu, mkweli na mwenye misimamo imara katika maamuzi yake. Mwandishi amemchora mhusika huyu kama kielelezo cha vijana wengi wanaokumbana na misukosuko mingi na mibaya kama siyo michungu katika maisha yao.

Kwanza kabisa kijana huyu anashindwa kuendelea na maisha ya masomo baada ya baba yake kufariki ghafla. Mungu hamtupi mja wake. Utubora anapata kazi ya ukarani katika kampuni ya tajiri Ahmed. Hapa Utubora anakuwa maarufu kuliko watu wote kwenye ofisi ya karafuu na matokeo yake analipwa mshahara mkubwa na kuwa gumzo Unguja nzima.

Akiwa katika ofisi yake bwana Ahmed, tajiri yake anakutana na sheha binti mrembo wa Ahmed. Kutokana na usuhuba uliokuwapo baina Ahmed na baba yake Utubora, posa ya utubora kwa sheha inakubaliwa. Lakini kama wasemavyo wahenga mkamia maji hanywi. Wakati Utubora anapanga ndoa, vita vinatokea na serikali inatoa wito kwa vijana kujitokeza kwenda Burma kupigana. Naye anakuwa miongoni mwa vijana hao. Akiwa vitani Sheha anapata mchumba kijana tajiri na kuamua kuolewa naye. Habari hii inamsikitisha Utubora. Kijana anakata tama na kukaribia kuyakatisha maisha yake.

Anaporudi Unguja anaona kazi ya ofisini haimpi furaha wala amani. Licha ya mshahara wake kuongezwa anachukuwa maamuzi magumu ya kuacha kazi ya kuajiriwa. Tajiri yake anambembeleza asiache kazi na kuahidi kumuongeza mshahara lakini anakataa. Hata mtumishi wake wa nyumbani, Bi anajaribu kumkanya Utubora kutoacha kazi. Utubora anashikilia kuacha kazi ya kuajiliwa na kwenda kijijini kuwa mkulima.

Utubora anahamia Busutamu, kijiji alichozaliwa na kukulia mama yake. Anajenga nyuma nzuri na afuga kuku kwa msaada wa Bihaya mtumishi wake. Utubora anakubalika kijijini hapo kutokana na busara yake huruma na na uchapakazi.

Pamoja na furaha kubwa aliyopata, Utubora anashindwa kuvumilia baada ya kupata taarifa kuwa Bimkubwa amekataa kuonana wala kuongea na watu wengine zaidi ya mwanakwao na mwanakwetu. Kwa busara na jitahada anafanikiwa kumrejeshea furaha Bimkubwa aliyoipoteza baada ya kufiwa na mume, watoto na mjukuu wake kipenzi. Kifo cha mjukuu wake kipenzi. Kifo cha mjukuu wa Bimkubwa kilimuumiza sana. Je unadhani ni kwa sababu gani kilimuumiza?

Maisha ya binadamu hayaishii katika kufanya kazi tu. Yapo mambo anuai anayohitaji binadamu kuyafanya. Jambo moja kubwa katika maisha mbali na kazi ni mapenzi. Mapenzi. Mapenzi yana nini? Mapenzi matamu ni yale yanayohusu pande mbili kwani mapenzi ya aina hiyo huleta ndoa yenye amani na utulivu. Ndoa ya upande mmoja ni hatari.

Baada ya Utubora kuachwa na sheha hakutaka kabisa kujihusisha na mapenzi na aliamua kukubali usemi wa Samaki mmoja akioza wote wameoza. Hata hivyo msimamo wake ulianza kulegea baada ya kukutana na radhia, binti mrembo mwenye upendo wa kweli. Lakini bahati mbaya, Radhia ana mchumba wake na mchumba mwenyewe ni rafiki mkubwa wa Utubora aitwaye Mkuu. Mkuu na Utubora ni marafiki tangu wakiwa chuoni. Mbaya zaidi, Radhia na Sheha, mchumba wa kwanza wa Utubora, ni mabinamu, bila kujua utubora anapendwa na Radhia kiasi cha Radhia kuvunja uchumba wake na Makuu

Katika vurugu hiyo ya kuvunjwa kwa uchumba, Makuu anadhani Utubora anahusika. Lakini bahati Utubora hajui. Utubora anaitwa kurejea kwa mwajiri wake. Sheha anatumia nafasi hiyo kuhakikisha kuwa Utubora anakuwa mume wake kwani ndoa ya Sheha imevunjika. Nini kitatokea kwa Radhia kuhusu pendo lake kwa Utubora? Je Utubora atakubali kumsaliti rafikiyake Makuu? Vipi kuhusu Bimkubwa jambo gani lilimpata? Na Sheha je, alifanikiwa? Fuatana na mwandishi wa riwaya hii ili uweze kujua jinsi nguvu ya mapenzi ilivyo.

COMMUNITY REVIEWS

There are no reviews for this book yet

Write a Review