
No video uploads for Pius B. Ngeze |
Siri ya Binaadamu Kuishi Miaka Mingi
Kitabu hiki kimezingatia mapinduzi ya Sayansi na Teknolojia, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Matibabu na uelewa uliopo duniani kuhusu elimu mpya ya kumwezesha binadamu kuishi miaka mingi. Ni kitabu cha aina yake ambacho kila mwanadamu anayependa kuishi miaka mingi anapaswa kukimiliki, kukisoma na kukirejea mara kwa mara.
|
|
Jifunze Kustawisha Mboga
Kitabu hiki kimeandikwa ili kiwasaidie Wakulima, Maofisa Ugani, Wanafunzi na Wanavyuo kuanzisha aina mpya ya kilimo, yaani, Ustawishaji wa Mbogamboga. Kutokana na wingiwa aina za mbogamboga zilizopo, kitabu kimeandikwa kwamuhtasari.
|
|
Jifunze Kustawisha Uyoga
Uyoga ni zao la viumbe hai viitwavyo kuvu. Kwa watu wengi hapa nchini Uyoga unaofahamika ni ule unaookotwa au unaoonekana ukiota porini au kwenye vichuguu wakati wa msimu wa mvua. Ukiwaeleza kuwa uyoga hustawishwa kama ilivyo kwa mazao mengine, hawakuelewi!
|
|
Kanuni za Ukulima wa Kisasa
Kanuni za Ukulima wa Kisasa ni kitabu kinachoeleza Kanuni Ishirini na Tano (25) za Ukulima wa Kisasa. Kanuni hizo ni zile ambazo wakulima wanapaswa kuzisoma na kuzielewa kwa lengo la kuendesha kilimo cha kisasa cha mazao mbalimbali ya kilimo. Kanuni hizo zimeelezwa kwa kikamilifu kitabuni.
|
|
Kilimo Bora cha Maharage
Kilimo Bora cha Maharage ni kitabu kinachoeleza asili, historia, umuhimu wake, sehemu kuu za mmea, aina na jinsi ya kulistawisha kisasa ili kuongeza mavuno kutoka magunia mawili kwa hekta hadi zaidi ya magunia kumi na moja kwa hekta.
|
|
Kilimo Bora cha Mahindi
Kilimo Bora cha Mahindi ni kitabu kinachoeleza mambo mbalimbali yanayohusu mahindi: asili yake, ustawishaji, ulinzi, uvunaji na hifadhi yake. Mahindi ni nafaka muhimu nchini. Hutumiwa na wananchi wengi kwa chakula, kuuza na kutengenezea pombe. Watu wengi hupenda kula ugali wa mahindi. Ni mtamu na huleta afya. Lakini, watu wachache wanaojua jinsi ya kustawisha vizuri zao hili. Kitabu hiki kitakuwa cha msaada kwa wakulima, maofisa ugani, wanafunzi na wanavyuo.
|
|
Kilimo Bora cha Muhogo
Kilimo Bora cha Muhogo ni kitabu ambacho kinaeleza asili, aina, historia ustawishaji Muhogo.
|
|
Kutengeneza na Kutumia Mboji Katika Kilimo
Kitabu hiki kinahusu Mbolea za Asili. Mbolea za asili hutokana na viumbe hai, yaani, wanyama na mimea. Virutubisho vilivyo katika mbolea hizi vilitumika kwanza katika kustawisha mimea hiyo au katika kulisha wanyama hao
|
|
Migomba Uanzishaji na Utunzaji wa Shamba
Migomba: Uanzishaji na Utunzaji wa Shamba ni kitabu kinachofundisha mkulima mpya, na hata mwenye uzoefu, namna ya kuanzisha shamba jipya la migomba na kulitunza vizuri. Kitabu kinaeleza pia asili na historia ya zao hili, botania ya mmea, uvunaji na uuzaji wa ndizi. Kitabu hiki kimegawanyika katika sura kumi zifuatazo:
|
|
Misingi ya Kilimo Bora
Ili tuweze kuleta Mapinduzi ya Kijani nchini, lazima kilimo chetu kihame kutoka Kilimo cha Mazoea ambacho kimetumika tangu mababu na mababu, karne na karne na kuwa Kilimobiashara.
|
|
Mwongozo wa Kilimo Bora cha Alizeti
Alizeti ni moja ya mazao makuu ya biashara yanayostawishwa hapa nchini. Mbegu zake hutoa mafuta asilimia 35-45 na mashudu yake hutumika kulisha mifugo. Mafuta daraja la kwanza hutumika kupikia chakula cha binadamu na ya daraja la pili hutumika viwandani kutengeneza bidhaa mbalimbali kama vile sabuni, rangi, vipodozi mbalimbali n.k.
|
|
Utengenezaji na Matumizi ya Mboleavunde Katika Kilimo
Mboleavunde ni mbolea inayotengenezwa na wakulima kutokana na masalia ya mimea na wanyama ambayo yameozeshwa na vidubini vilivyo katika rundo. Rundo hilo ni mchanganyiko wa masalia mengi ya mimea na wanyama na katika mahali padogo ambapo vitu hivyo huoza kwa muda mfupi
|
|
Jifunze Kustawisha Viazi Mviringo
Katika kundi la mazao ya mizizi, Viazi Mviringo ni maarufu na vina umuhimu wa pekee.Ni zao la chakula na biashara katika nchi nyingi zilizoendelea na zinazoendelea. Zao hili nimoja ya mazao manne yachakula yanayozalishwa kwawingi na kutumiwa na watu wengi duniani.
|
|
Visumbufu Vya Mazao Shambani
Visumbufu vya Mazao Shambani ni kitabu kinachoeleza visumbufu vinavyoshambulia mimea ya mazao ikiwa shambani. Visumbufu hivyo ni vingi, lakini, vinavyozungumzwa kitabuni ni vile muhimu zaidi. Kitabu kimegawanyika katika Sura sita zifuatazo:
|
|
Uboreshaji wa Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji
Uboreshaji wa Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji ni kazi inayohitaji Maarifa na Juhudi ili kupata mazao mengi na yaliyo bora. Wanunuzi hupenda kuku bora, mayai bora na nyama bora ambayo hupatikana kutokana na juhudi ya mfugaji kuweza kuwatunza kuku wake ipasavyo. Ufugaji bora wa kuku humhitaji mfugaji kuelewa na kuzingatia kanuni za ufugaji bora kuku. Ni lazima mfugaji wa kuku wa kienyeji awe na elimu hii ili aweze kuendesha shughuli zake kwa usahihi na kwa manufaa ya wateja.
|
|
Ufugaji Bora wa Kuku
Ufugaji bora wa Kuku ni kitabu kizuri ambacho kimetayarishwa kwa makini kwa ajiliya watu ambao tayari wanafuga kuku wa kienyeji na wakigeni (kuku chotara) na wale ambao wangependa kuanza ufugaji wa kisasa wa kuku
|
|
Mwongozo wa Ufugaji Bora wa Nyuki
Mwongozo wa Ufugaji Bora wa Nyuki ni kitabu kinachotoa maelezo kuhusu jamii ya nyuki, namna ya kuwafuga, kurina asali, utunzaji na uuzaji wa asali na nta.
|
|
Mwongozo wa Ufugaji Bora wa Samaki
Mwongozo wa Ufugaji Bora wa Samaki ni kitabu kinachoeleza namna ya kufugasamaki nchi kavu kwa kutumia mabwawa. Ufugaji wa samaki huweza kumletea mkulima fedha nyingi kuliko watu wanavyofikiri.
|
|
Jifunze Ufugaji Bora wa Nguruwe
Jifunze Ufugaji Bora wa Nguruwe ni kitabu kinachowalenga wafugaji wa nguruwe wa aina kuu tatu zifuatazo:Wafugaji wenye uzoefu mdogo.Wafugaji wa ngazi ya kati wanaoinukia katika ufugaji wa kisasa na wa kibiashara na Wafugaji wakubwa wanaofuga nguruwe kisasa kwa ajili ya kupata faida kubwa. Wafugaji wadogo wanaoanza au waliokwishaanwenza mtaji mdogo au hawana mtaji kabisa na wanaweza kufuga nguruwe na watangundua kuwa ufugaji huu una faida kubwa. Kinunue kitabu hiki ili uelekee kwenye ufugaji wa kisasa na wa kibiashara.
|
|
Magonjwa ya Mifugo
Magonjwa ndicho chanzo kikuu cha vifo vya mifugo na umaskini wa wafugaji. Maelfu ya mifugo hufa kila mwaka kutokana na magonjwa. Bila kuugua, mifugo haiwezi kufa .Dhibiti magonjwa ya mifugo ili kuongeza uzalishaji wa maziwa, nyama, mayai, ngozi n.k. na kuondoa umaskini wa wafugaji. Moja ya Kanuni za Ufugaji Bora inawataka wafugaji wadhibiti magonjwa ya mifugo. Lakini, magonjwa yana visababishi au wakala. Tukijua visababishi hivyo na namna ya kuvidhibiti au kuvipunguza, magonjwa yatapungua . Magonjwa yanazuilika. Magonjwa yanatibika. Tufanye, basi, kazi hizo mbili ili kuboresha ufugaji. Lengo kuu la kitabu hiki ni kuwasaidia wafugaji wafanye hivyo.
|
|
Mwongozo wa Ufugaji Bora wa Mbuzi
Mwongozo wa Ufugaji Bora wa mbuzi ni kitabu ambacho kinaeleza namna ya kisasa ya kufuga mbuzi na kupata faida kubwa kutokana na ufugaji huo
|
|
Silaha Mia Moja za Kiongozi
Kiongozi ni mtu yeyote, mwanamke au mwanaume, mwenye madaraka au mamlaka juu ya mtu mmoja au watu wengi. Maana nyingine ya Kiongozi ni mtu aliyepewa jukumu la kuongoza mtu mmoja au watu wengi. Mtu mmoja huyo anaweza akawa mwanandoa mwenzie au mtu mmoja mwingine ambaye ana ushirika naye.
|
|
The One Hundred Weapons for a Leader
A leader is any person, a man or woman, with power or authority over one or more people. Another meaning of a leader is a person who was given an authority to lead a single person or many people. That single person may be a fellow matrimonial partner or a fellow person whom you co-operate with. “Many people” may start from his/her family members up to the whole nation.
|
|
No award found
Ask Pius B. Ngeze anything
No questions, Be the first to ask Pius B. Ngeze
Contact Form