Siri ya Binaadamu Kuishi Miaka Mingi
Publisher
Tanzania Educational Publisher
Language
Swahili

Rent This Book

Expires on August 02, 2025

TSh 4,000/=

Choose Option

BOOK OVERVIEW

Ndugu Pius Bakengera Ngeze (pichani), katika kitabu hiki, Siri ya Binadamu Kuishi Miaka Mingi: Nguzo 72 Zinazoshikilia Uhai Wako, ametumia uzoefu wa umri wake, uandishi na usomaji wa vitabu na machapisho mengine kuwaandikia Wosia binadamu kuhusu jinsi ya kuishi miaka 80-100. Kitabu hiki kimezingatia mapinduzi ya Sayansi na Teknolojia, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Matibabu na uelewa uliopo duniani kuhusu elimu mpya ya kumwezesha binadamu kuishi miaka mingi.

Ni kitabu cha aina yake ambacho kila mwanadamu anayependa kuishi miaka mingi anapaswa kukimiliki, kukisoma na kukirejea mara kwa mara.

Siri ya Binadamu Kuishi Miaka Mingi iko ndani ya kitabu hiki. Kwa hiyo, ni muhimu ukisome ili uweze kuigundua. Uhai ulionao leo ni zawadi kuu kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Jukumu lako ni kufanya uamuzi wa kuutunza (uhai huo) kwa kipindi kirefu kadiri inavyowezekana au kwa kipindi kifupi. Si jukumu lake, ni jukumu lako. Ukipewa zawadi na mtu anayekuthamini au anayekupenda, ni jukumu lako kuitunza vizuri ili iweze kukufaa kwa kipindi kirefu au kutoitunza na matokeo yake utaifaidi kwa kipindi kifupi. Hali ndivyo ilivyo kwa zawadi ya uhai tuliyopewa na Mungu.

Kila mtu anapenda kuishi miaka mingi na iwe ya furaha, isiwe ya dhiki, shida na afya mbaya kwa kipindi kirefu. Lakini, hayo ni matarajio na matumaini tu.

Pamoja na kujitahidi kutekeleza Nguzo hizo, endelea Kumtegemea na Kumwomba msaada Mungu. Bila yeye huwezi kitu. Kwake hakuna lisilowezekana.

COMMUNITY REVIEWS

There are no reviews for this book yet

Write a Review