Uchambuzi wa Sera, Uongozi na Maslahi ya Watanzania
Publisher
E & D Vision Publishing
Language
Swahili

Rent This Book

Expires on August 11, 2025

TSh 3,000/=

Choose Option

BOOK OVERVIEW

Uchambuzi wa Sera, Uongozi na Maslahi ya Watanzania ni mkusanyiko wa makala mbalimbali yanayotetea na kupigania maslahi ya Watanzania katika uporwaji wa rasilimali na haki za watu za msingi. Chachage anafanya hivyo kwa kuelezea na kupambanua kwa kina masuala yanayohusu sera, uchumi, utamaduni na siasa. Anauweka uchambuzi wake katika muktadha wa Utandawazi, anaouita utandawizi, ambao ni mwendelezo wa ukoloni na ukoloni mamboleo na “daima unalenga kujenga uhusiano wa kinyonyaji uliojikita katika uporaji wa ardhi na rasilimali, ulazimishaji wa wazalishaji kuzalisha mali na bidhaa za kukidhi mahitaji ya watu wa Magharibi na uwepo wa soko la wafanyakazi wa ujira duni...” Madhumuni ya uchambuzi wa masuala haya, ambayo ameyaelezea katika lugha nyepesi, yanalenga kutofautisha ukweli na uongo katika mambo mengi wanayoambiwa na kutokea Watanzania, ili msomaji aweze kuona ni kwa nini maendeleo ya Watanzania yamekuwa kitendawili. Hiki ni kitabu cha kusomwa na kila Mtanzania, kwani masuala anayozungumzia Chachage yanamgusa kila Mtanzania.

COMMUNITY REVIEWS

There are no reviews for this book yet

Write a Review