
BOOK OVERVIEW
Hadithi hizi ni matunda ya shindano la Fasihi lililoshirikisha wanafunzi 40 kutoka shule 10 za Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe na hadithi za washindi watatu zimetumika kufanya mkusanyiko na kutengeneza kitabu hiki. Shindano liliandaliwa na Taasisi ya Tanzania Fasihi Fund (TAFF) mwaka 2021. Hadithi zote zilibeba Kichwa cha habari kimoja ila ubunifu ndio umeleta tofauti kutoka hadithi moja mpaka nyingine, hata hivyo ili kunogesha utamu, Mlezi wa Fasihi Gwiji Mwamwingila wa Mtalimbo Books, aliamua kuzipa majina hadithi hizi ambapo zote awali zilikuwa na jina linalofanana mpaka nukta kwa kuwa ni zao la utunzi elekezi. TAFF iliamua kuendesha mashindano hayo na baadaye Tamasha la Fasihi ya Kiswahili ili kuwa na jukwaa linaloshiriki sio tu kukuza maarifa ya jamii, bali pia kuwa sehemu ya kukabiliana na changamoto za kimaendeleo kwa kutumia Fasihi Andishi na Fasihi Simulizi na kazi hii iliyopo mikononi mwako ni matunda yake