BOOK OVERVIEW
Katika kundi la mazao ya mizizi, Viazi Mviringo ni maarufu na vina umuhimu wa pekee.Ni zao la chakula na biashara katika nchi nyingi zilizoendelea na zinazoendelea. Zao hili nimoja ya mazao manne yachakula yanayozalishwa kwawingi na kutumiwa na watu wengi duniani. Mbali na utamu wa Viazi Mviringo, lakini, mlaji hujipatia asilimia kubwa ya chakula chenye asili ya wanga. Aidha,vina kiasi chakutosha cha protini,madini,vitamini namaji.
Umaarufu wake unaongezeka kila kukicha.Watoto,vijana na watuwazima hupenda kula viazi mviringo kama chipsi,viazi vilivyo pondwapondwa,viazi vilivyochemshwa n.k “Chipsi na kuku”,chipsi na mayai”,“chipsi na nyama” au “chipsi kavu” ni majina maarufu sana katika familia nyingi, migahawa, hoteli, mamalishe n.k.,h asahasa, kwa watoto,vijana na watuwasiokuwa na mudawakusubiri vyakula vinavyochukua muda mrefu kuviandaa.Kwasababu hii,mahitaji ya zao hili ni makubwa sana na bei yake huongezeka mara kwa mara.Lengo la kitabuhiki ni kuwawezesha wakulima wengi zaidi walistawishe kwakufuata kanuni bora, wajue jinsi yakulitayarisha na kulisindika.