Utengenezaji na Matumizi ya Mboleavunde Katika Kilimo
Publisher
Tanzania Educational Publisher
Language
Swahili
BOOK OVERVIEW
Mboleavunde ni mbolea inayotengenezwa na wakulima kutokana na masalia ya mimea na wanyama ambayo yameozeshwa na vidubini vilivyo katika rundo. Rundo hilo ni mchanganyiko wa masalia mengi ya mimea na wanyama na katika mahali padogo ambapo vitu hivyo huoza kwa muda mfupi. Kimuundo, rundo hilo limetengenezwa kutokana na tabaka za vitu vya kuozeshwa, samadi, majivu na udongo. Kitabu hiki kinahusu namna ya kutengeneza mboleavunde iliyo nzuri na namna ya kuitumia shambani. Kitabu kimetengwa katika sura sita zifuatazo:
- Udongo
- Mbolea
- Sababu ya kutumia masalia ya mimea na wanyama kutengeneza mboleavunde.
- Misingi ya utengenezaji wa mboleavunde.
- Muundo wa rundo na njia kuu za kutengeneza mboleavunde.
- Muhtasari, sifa, faida na matumizi ya mboleavunde.