
SHAABAN ROBERT SEHEMU YA KWANZAIkbar Shaaban Robert mtoto wa mwandishi nguli wa fasihi ya kiswahili Shaaban Robert ambaye alisha tawafu dunia, hapa Ikbar anatoa historiya ya Baba yake.
|
|
SHAABAN ROBERT SEHEMU YA PILIIkbar Shaaban Robert akiendelea kutoa historia ya maisha ya baba yake safari zake. n.k
|
|
SHAABAN ROBERT SEHEMU YA TATUIkbar Shaaban Robert akitoa shukrani zake kwa UNESCO kwa siku ya kiswahili duniani, lakini pia anatoa maoni yake juu ya tuzo kwaajili ya baba yake Shaaban Robert.
|
|
Ashi Kitabu Hiki
Hii ni diwani yenye mashairi mbalimbali yanayojadili mambo tofauti ya maisha ya binadamu. Kitabu hiki kimepewa jina, Ashiki Kitabu Hiki kwa lengo la kumpa msomaji hamasa ya kukisoma. Kwa kufanya hivyo, msomaji huyo atakuwa amefanikiwa kuyapata yote aliyokusudiwa kuyapata na hapo lengo la msanii litakuwa limetimia.
|
|
Insha na Mashairi
Maisha ya binadamu yamejaa changamoto nyingi. Binadamu hana budi kupambana na kutatua changamoto hizo. Katika kitabu hiki msanii anatoa mifano mbalimbali ya changamoto na jinsi ya kupambana nazo.
|
|
Koja la Lugha
Uhodari na utunzi mahiri wa Shaaban Robert unadhihirishwa katika kazi yake hii ya Koja la Lugha. Mashairi yaliyosukwa kwa ustadi na kwa tunu za jamii yanakusanywa na kuunda kitabu hiki.
|
|
Mapenzi Bora
Kitabu cha Mapenzi Bora kinazungumzia suala mtambuka la mapenzi. Mwandishi anachora suala hili kwa kuonesha ni namna gani mapenzi yanaweza kuwa na matokeo hasi au chanya kulingana na aina ya mapenzi yenyewe.
|
|
Mashairi ya Shaabani Robert
Hii ni moja ya diwani fupi inayozungumzia namna bora ambayo wanajamii wanaweza kuhusiana na kujiletea maendeleo. Masuala mbalimbali kama vile dini, maadili na maisha kwa ujumla wake yanazungumziwa ipasavyo na mwandishi.
|
|
Masomo Yenye Adili
Kitabu hiki kimekusanya mambo mengi ya hekima. Ni kitabu ambacho kimejaa hadithi fupi zenye maonyo, ushauri, maelekezo na maadili mbalimbali yahusuyo maisha. Yapo mashairi yenye wingi wa hekima ndani yake ambayo sambamba na hadithi fupi yanafanya kazi ya kuadilisha jamii katika nyanja zote za maisha.
|
|
Mwafrika Aimba
Mwafrika Aimba ni diwani inayosawiri maisha ya mwanadamu. Mshairi ameonesha jinsi maisha yalivyo kwa Mwafrika. Anadokeza dhuluma, manyanyaso, unafiki, usaliti na maovu.
|
|
Utubora Mkulima
Hii ni riwaya inayozungumzia maisha ya kijana aitwaye Utubora. Kama jina lake lilivyo, kijana huyu anajipambanua kuwa ni mtu jasiri, imara, mvumilivu, mwaminifu, mkweli na mwenye misimamo imara katika maamuzi yake. Mwandishi amemchora mhusika huyu kama kielelezo cha vijana wengi wanaokumbana na misukosuko mingi na mibaya kama siyo michungu katika maisha yao.
|
|
Kielezo cha Fasili
Elimu iliyokita mizizi komavu juu ya masuala mbalimbali ya jamii inafafanuliwa katika kazi hii ya Shaaban Robert. Mwandishi anayaelezea mambo ya jamii kama yalivyo. Si yote ni matamu na si vyote ni machungu ni mchanganyiko wa vyote vinavyoifanya jamii kuitwa jamii.
|
|
Kufikirika
KUFIKIRIKA ni riwaya fupi inayotumia mandhari ya kufikirika lakini lakini maudhui yake yanasadifu maisha ya jamii za kiafrika kwa sehemu kubwa. Kwa kawaida ndoa katika jamii za kiafrika hazipo kwa ajili ya mume na mke kuishi pamoja tu bali ni kupata watoto. Watoto ndio furaha na faraja ya wanandoa. Kutokanana Imani hiyo, ndoa ya mfalme na malkia wa kufikirika inagubikwa na wingu la huzuni kuu kutokana na wao kuandamwa na ugumba na utasa. Kwa huzuni kuu, mfalme anaamua kumshirikisha waziri wake mkuu kuhusu kadhia hiyo ambapo uamuzi unafikiwa kuwa mfalme na malkia waaguliwe.
|
|
Kusadikika
Kusadikika ni riwaya fupi inayozungumzia athari za ujinga ,ubinafsi na tamaa mbaya za viongozi katika jamii. Mwandishi ametumia mandhari ya kufikirika yaani angani ilikuifanya hadhira yake isihoji mambo mengi kwani nchi hiyo imekosa mawasiliano ya ana kwa ana na nchi za jirani. Ujinga ni mbaya sana kwa watu wa kawaida lakini ni maafa makubwa ikiwa ujinga utakuwa ni wa kiongozi hasa aliye wa ngazi ya juu. Katika riwaya ,viongozi wa nchi ya Kusadikika wamepewa mamlaka makubwa kiasi kwamba chochote wakisemacho ni amri.
|
|
Maisha Yangu Baada ya Miaka Hamsini
Riwaya hii ni ya kitawasifu ambamo bingwa wa fasihi Afrika mashariki na kati, Shaaban Robert (kwa sasa marehemu) anasimulia maisha yake katika awamu mbili. Awamu ya kwanza inahusu maisha yake kabla ya umri wa miaka hamsini na ile ya pili inahusu maisha yake baada ya miaka hamsini hadi kustaafu kwake. Masimulizi haya binafsi yanaanzia katika mwaka wa 27 ya maisha mwandishi ambaye anadokeza kwa kifupi sana hamu kubwa san aliyokuwa nayo ya kuwa na heshima kubwa katika jamii. Aliamini kwa mtu asiye na jina (heshima) zuri basi mtu huyo ana ukiwa mkubwa sana duniani. Hamu yake ilikuwa ni kutokujihusisha na mapenzi kabla ya ndoa.
|
|
Siku ya Watenzi Wote
SIKU YA WATENZI WOTE ni riwaya ya kijamii inayojadili maisha ya wanadamu namna wanavyohusiana wao kwa wao na pia baina yao wao na Mungu. Ni riwaya inayozungukia kipindi cha mabadiliko katika nchi ya Tanganyika mara tu baada ya uhuru. Mabadiliko hayo yamegusia Nyanja mbalimbali za kisiasa, kiuchumi, kijamii na kitamaduni. Pamoja na mabadiliko hayo hasa ya kisiasa, tabaka la wenyenacho linaendeleza dhuluma, ufisadi, ukatili, uonevu na maovu mengine na kuwaacha watu wa tabaka la chini katika njaa kali, umasikini uliokithiri, makazi duni na kukata tamaa.
|
|
Tenzi za Marudi Mema na Omar Khayyam
Utungo huu umejaa tunu na mafunzo kwa jamii ukisawiri muelekeo wa jamii kwa kutoa miongozo itakayotumika kama reli za maisha ya kila siku. Marudi si marudi tu, bali yapaswa kuwa marudi mema yatakayokuwa msaada kwa jamii.
|
|
Wasifu wa Siti Binti Saad
Riwaya hii ya kiwasifu inazungumzia mwimbaji maarufu wa taarabu katika ukanda wa Afrika Mashariki naAfrika kwa ujumla. Mwandishi anatumia kalamu yake kueleza kwa kifupi maisha ya msanii huyo haikuwarahisi kwa mtu huyu mzawa wa Fumba kwa wazazi masikini sana, mmoja akiwa mkulima na mwingine mfinyanga vyungu. Siti binti Saad alizaliwa tarehe 08/03/1880 kijijini Fumba na alifariki mnamo tarehe 08/07/1950 akiwa na umri wa mika sabini
|
|
|
Adili na Nduguze
Kutokana na uadilifu wake, Adili anapendwa na jamii nzima. Binadamu kupendwa na wanadamu wenzake ni jambo la kawaida lakini kupendwa na kuheshimiwa na viumbe wengine kama majini ni jambo lisilo la kawaida. Mfalme Rai wa nchi ya ughaibu naAdili, liwaliwa Janibu walipendwa na kuheshimiwa na binadamu pamoja na majini
|
|
Almasi za Afrika
ALMASI ZA AFRIKA Ni mkusanyiko wa mashairi, riwaya na tenzi nyingi zenye wingi wa hekima na maadili mema kuhusu maisha ya binadamu. Mwandishi Shaaban Robert anayatazama maisha katika Nyanja zote kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni. Kwa ujumla ameyatafakari maisha na kuyaona kuwa yamejaa mambo mengi, mema na mabaya.
|
|
Pambo la Lugha
Pambo la Lugha ni mkusanyiko wa mashairi ya Shaaban Robert unaoakisi maisha ya jamii kwa kuangazia nyanja mbalimbali na mabadiliko yake. Diwani hii pendwa imedhihirisha umaarufu na utamu wake kwa kutajwa na kunukuliwa katika majukwaa mbalimbali ya wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili.
|
|
No award found
Ask Shaaban Robert anything
No questions, Be the first to ask Shaaban Robert
Contact Form