Wasifu wa Siti Binti Saad
Publisher
Mbiu Press
Language
Swahili

Rent This Book

Expires on August 02, 2025

TSh 2,000/=

Choose Option

BOOK OVERVIEW

Riwaya hii ya kiwasifu inazungumzia mwimbaji maarufu wa taarabu katika ukanda wa Afrika Mashariki naAfrika kwa ujumla. Mwandishi anatumia kalamu yake kueleza kwa kifupi maisha ya msanii huyo haikuwarahisi kwa mtu huyu mzawa wa Fumba kwa wazazi masikini sana, mmoja akiwa mkulima na mwingine mfinyanga vyungu. Siti binti Saad alizaliwa tarehe 08/03/1880 kijijini Fumba na alifariki mnamo tarehe 08/07/1950 akiwa na umri wa mika sabini

Maisha yake ya awali hayakuwa mazuri hata kidogo. Wazazi wake walikuwa ni waafrika wa makibila mawili tofauti. Baba yake alikuwa mnyamwezi na mama yake alikuwa ni mzigua, wote wazaliwa wa kisiwa cha unguja . Siti Binti Saadaliishi katika zama mbili tofauti. Zama ya kwanza aliishi kwa dhiki kubwa sana akiwa ni msaidizi wa mama yake kuuza vyungu na alijulikana kwa jina la mtumwa binti Saad. Katika kipindi hicho alijaliwa kupata mume ambapo walijaliwa mtoto mmoja.

Sinti binti saad alizaliwa pamoja na ndugu waume wawili yaani kaka zake, Musa na Mbaruku na pia dada yake masika. Siti hakusoma. Zama yake ya pili inahusu kipindi cha miaka thelathini na tisa, kipindi ambacho jina la Siti Binti Saad liliibuka na kuvuma kama upepo wa kusi.

Kila mtu ana bahati yake kipawa ama kipaji chochote kikipata mtu mwema wa kukiendeleza huvuka vikwazo vyote. Mtumwa wakati akiuza vyungu vya mama yake alikuwa akinadi vyungu hivyo kwa kuimba nyimbo mbalimbali. Sauti yake tamu iliwavutia watu kununua vyungu japo vyungu hivyo havikuwa vizuri. Sauti yake tamu ilifunika ubaya wa sura yake. Bidii yake ilimuongoza katika kutafuta mafanikio zaidi akaamua kuhamia mjini.

Maisha hutafutwa. Waswahili hudai kuwa mbwa hafi maji akiuona ufuko. Aliopofika mjini, siti alionana na mwalimu Mhisin Ali. Huyu ndiye aliyemuibia siti kweli kutoka mtumwa binti Saad. Ali Muhsin alinufaika kwa kumpata Siti na kasha akamwingiza katika taarabu hadi kufika kuwa malkia wa taarabu Afrika akizidiwa na mwimbaji maarufu wa misri.

Je, Siti binti Saad aliwezaje kufikia ustawi wa hali ya juu kiasi hicho? Changamoto mbalimbali alizokutana nazo alizitatuaje? Je, wapinzani wake walimwacha hivi hivi? Riwaya hii inayo majibu yote na zaidi. Fuatana na mwandishi ili uweze kubaini yote yaliyompata mwimbaji huyu.

COMMUNITY REVIEWS

There are no reviews for this book yet

Write a Review