Maisha Yangu Baada ya Miaka Hamsini
Publisher
Mbiu Press
Language
Swahili

Rent This Book

Expires on August 02, 2025

TSh 2,000/=

Choose Option

BOOK OVERVIEW

Riwaya hii ni ya kitawasifu ambamo bingwa wa fasihi Afrika mashariki na kati, Shaaban Robert (kwa sasa marehemu) anasimulia maisha yake katika awamu mbili. Awamu ya kwanza inahusu maisha yake kabla ya umri wa miaka hamsini na ile ya pili inahusu maisha yake baada ya miaka hamsini hadi kustaafu kwake. Masimulizi haya binafsi yanaanzia katika mwaka wa 27 ya maisha mwandishi ambaye anadokeza kwa kifupi sana hamu kubwa san aliyokuwa nayo ya kuwa na heshima kubwa katika jamii. Aliamini kwa mtu asiye na jina (heshima) zuri basi mtu huyo ana ukiwa mkubwa sana duniani. Hamu yake ilikuwa ni kutokujihusisha na mapenzi kabla ya ndoa. Shida ikwa kumpata mwenza sahihi. Lakini kama walivyosema, atafutaye hachoki alifanikiwa kumpata mke sahihi. Wema hawana maisha ni msemo unaoweza kuonekana kutokuwa na uzito lakini ndivyo maisha yalivyo. Amina, mke wa Shaaban Robert, mwandishi wa riwaya hii alidumu kwa miaka kumi tu katika ndoa akafariki huku akiacha watoto wawili, mwana na binti. Ni pigo kubwa kwa Shaaban Robert kifo ni faradhi lakini mauko hayajawahi kuzoeleka. Pigo hili lilimuacha mume katika simanzi kuu. Hakuvumilia kukaa kimya. Akaamua kutunga shairi la kumlilia mkewe, Amina. Ni nini kilicho ndani ya shairi hilo? Upweke unasumbua, Shaaban Robert alishindwa kuishi maisha ya upweke. Baada ya miaka saba ya ujane aliamua kuoa mke wa pili. Aliyekosa titi la mama la mbwa huamwa. Hakuwa na chaguo lingine, istoshe watoto wake walihitaji malezi bora, figa moja haliinjiki chungu. Kama mzazi anyeyajua majukumu yake, Shaaban Robert anawakalisha watoto wake mmoja baada ya mwingine na kuwapa nasaha bora ambazo zitawasaidia katika maisha yao ya baadae. Ni zipi nasaha hizo? Kazini, Shaaban Robert alikuwa hodari wa kazi, mchapakazi, mwaminifu na mkweli na aliyetimiza majukumu yake kikamilifu kutoka idara ya forodha, utunzaji wa wanyama na idara ya utawala. Watumishi wenzake wote walipofanya makosa walielekezwa kuiga mfano mzuri Shaaban Robert. Huyu mtu alikuwa ni wa aina gani? pamoja na mzuri yote aliyoyafanya Shaaban Robert parikuwa na dosari moja huko ofisini. Ubaguzi wa rangi. Kuanzia kuaminika, kuorodheshwa katika hati na katika usafiri, mtu mweusi hakupewa nafasi anayostahili. Shaaban Robert aliyavumilia yote haya. Baada ya misukosuko mingi ya maisha Shaaban Robert anaamua kuwa mwandishi wa kazi mbalimbali za kifasihi. Anapata upinzani mkubwa sana kutoka kwa wakinzani wake lakini anapata watetezi wengi vilevile kazi zake zinapitia changamoto mbalimbali hasa kupitia vuguvugu la harakati za ukombozi wa kisiasa katika nchi za Afrika mashariki pia vita kuu ya pili ya dunia. Uandishi wake unakumbwa na changamoto kuwa za kimaslahi. Wapigishaji chapa wanamdhurumu sana. Lakini alidhamiria na kama tujuavyo, penye nia pana njia, Shaabani Robert hakukata tamaa. Aliwezaje kufanikisha uchapishaji wa vitabu vyake zaidi ya ishirini sita katika hali ya dhuluma kubwa hivi? Riwaya hii ina majibu mujarabu. 

COMMUNITY REVIEWS

There are no reviews for this book yet

Write a Review