MWAMWINGILA G.P

BIOGRAPHY




No video uploads for Mwamwingila G.P
Babu Yangu Anajua Kila Kitu

Hadithi hii nimeitunga kwa mwanangu Odilia Goima Mwamwingila, ambaye anapenda sana kuniuliza maswali, nampenda Odilia kwa kuwa anapenda kujua vitu vingi.


  • Published : May 26, 2024

Chifu Mtalimbo Kiboko ya Mamba

Natabaruku hadithi hii kwa Dkt. Bryan Mtalimbo Mwamwingila, ambaye aliomba zawadi ya hadithi ili asome katika siku yake ya kuzaliwa mwaka 2020.


  • Published : June 3, 2024

Gian na Siafu

Hadithi hii nimeitunga maalumu kama zawadi kwa mwanangu Gian Goima Mwamwingila, ambaye amekuwa akiniganda muda ninapoandika, mimi nikiandika yeye anabonyeza vitufe vya kompyuta mpakato yangu. Sasa nimeona bora nimuandikie hadithi hii ili atakapoanza kusoma basi asome na ujumbe huu


  • Published : June 3, 2024

Kisa cha Panzi na Kunguru

Hadithi hii nimeitunga kama zawadi maalumu kwa Watoto wa Afrika, wapate kutambua umuhimu wa utawala bora, kupendana, kuaminiana na kushirikishana katika maamuzi yenye manufaa kwa mataifa yao na bara zima la Afrika.


  • Published : June 5, 2024

Kisa cha Punda na Pundamilia

Hadithi hii nimeitunga maalumu kama zawadi kwa mbuga ya wanyama ya Mikumi, Morogoro. Mapenzi yangu kwa Mikumi hayana kipimo, mara zote nikiwa Mikumi ninapata furaha sana, nafsi yangu hupata utulivu mkubwa na akili yangu hupata mawazo mapya yenye kunifanya kugundua uzuri wa nchi tajiri kwenye sekta ya maliasili na utalii, si nyingine bali Tanzania.


  • Published : June 5, 2024

Kisa cha Simba Mtu

Hadithi hii nimeitunga maalumu kama zawadi kwa rafiki zangu wa Mtwara, walionipokea na kunitembeza maeneo mbalimbali na huko nilipata visa vingi kikiwemo kisa hiki cha Simba Mtu.


  • Published : June 5, 2024

Majuto ya Kudumu

Hadithi hizi ni matunda ya shindano la Fasihi lililoshirikisha wanafunzi 40 kutoka shule 10 za Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe na hadithi za washindi watatu zimetumika kufanya mkusanyiko na kutengeneza kitabu hiki.


  • Published : June 6, 2024

Mama the Engine I Know

ama the Engine I Know is a celebratory tribute to motherhood. Hawa Hussein Kayanda, a budding brilliant poet, gives us a refreshing and humble submission of a grateful daughter to an alter ego mother in this first publication of her poetry.


  • Published : June 6, 2024

Mapenzi Yamelogwa

Riwaya hii niliitunga mwaka 2002 wakati huo nikimuuguza marehemu mama yangu Bi. Hawa Ally Rwazihonda aliyefariki dunia Desemba 24’ 2002. Mola amlaze mahala pema peponi. Wakati nikiitunga nilidhamiria itoke katika gazeti la Ijumaa na baadae Mwananchi, lakini kutokana na sababu mbalimbali haikuweza kutumika.


  • Published : June 6, 2024

McHezo wa Yai

Hadithi hii ni kwa ajili ya watoto wote wapenda michezo. Mchezo wa kukimbia na yai mdomoni ni mchezo rahisi kuchezwa katika mazingira yoyote. Ni mchezo unaoongeza ari ya ushindani baina ya watoto kadhalika umakini katika maisha ya mtoto ya kila siku. Tuwafunze watoto kucheza bila hofu kwani unaweza kuwapatia mayai yaliyochemshwa na mwisho wakapata kula mayai hayo hayo na hivyo kupata vyote yaani furaha ya mchezo na afya ya mwili.


  • Published : June 6, 2024

Rafiki Yangu Kipepeo

Hadithi hii nimeitunga mahususi kwa watoto wanaopenda kupata maarifa ya michezo iliyochezwa miaka ya zamani na kwa sasa imeanza kupotea. Kipindi ambacho uoto wa asili ulitamalaki kila pahala, ila kwa sasa ni aghalabu sana na hivyo watoto wanakosa wasaa wa kushiriki michezo inayogusa viumbe asili na halisi. Ama kwa nafasi nyingine nimemulikia maeneo ya hifadhi za taifa ambapo asili imehifadhiwa na hivyo watoto wapate kuwashawishi wazazi na walezi kuwapeleka katika maeneo hayo ili nao wakafaidi michezo inahusisha viumbe asilia.


  • Published : June 6, 2024

Zawadi Yenye Shaka

Hadithi hizi ni matunda ya shindano la fasihi lililoshirikisha wanafunzi arobaini kutoka shule kumi za sekondari za wilaya ya Kisarawe na hadithi za washindi watatu zimetumika kufanya mkusanyiko na kutengeneza kitabu hiki.


  • Published : June 6, 2024

Bima ya Penzi

“Mwamwingila G.P ni mwandishi bora wa fasihi katika karne ya 21, baba wa watoto zaidi ya kumi na wajukuu lukuki wa kifasihi niliopata kuwafahamu. Mwamwingila ni mwalimu na mshauri mahiri, akiongoza waandishi chipukizi katika kuunda hadithi kwa zaidi ya miaka kumi na mitano.


  • Published : October 9, 2024


No award found

Ask Mwamwingila G.P anything

Contact Form