
BOOK OVERVIEW
Hadithi hii nimeitunga kwa mwanangu Odilia Goima Mwamwingila, ambaye anapenda sana kuniuliza maswali, nampenda Odilia kwa kuwa anapenda kujua vitu vingi. Odilia husema ya kuwa, anapenda kuwa Mtaalamu wa Masuala ya Usafiri wa Anga, wakati huo huo anapenda kuchora na kubuni mitindo ya mavazi. Sisi kama wazazi wake tunamtakia kheri katika yote anayopenda, kwani hakuna linaloshindikana duniani. Nia thabiti, bidii binafsi na mwongozo bora, kila jambo litawezekana. Kitabu hiki pia kiwafikie watoto wa rika na masomo mbalimbali. Wote kwa pamoja wanaweza kupata kuijua nchi yetu ya Tanzania na wakati huo huo wakifurahia utashi na ucheshi wa Babu. “Babu yangu, anajua kila kitu.” Kitabu hiki kiwape watoto wote, mwanga wa mambo mengi na mazuri katika nchi yetu ili wapate hamasa ya kutembea sehemu mbalimbali na kujionea mwenyewe uzuri na utajiri wa nchi ya Tanzania.