Bima ya Penzi
Publisher
Mtalimbo Books
Language
Swahili
BOOK OVERVIEW
“Mwamwingila G.P ni mwandishi bora wa fasihi katika karne ya 21, baba wa watoto zaidi ya kumi na wajukuu lukuki wa kifasihi niliopata kuwafahamu. Mwamwingila ni mwalimu na mshauri mahiri, akiongoza waandishi chipukizi katika kuunda hadithi kwa zaidi ya miaka kumi na mitano.
Kupitia riwaya hii, nimeweza kumfahamu zaidi kwa kuwa ameonesha mambo makubwa ya sasa na kutabiri yajayo. Huu ni uwezo wa kipekee sana. Naweza kukiri ya kuwa sijawahi wala sitarajii kuona kitabu chenye nguvu ya burudani, ushawishi na utabiri wa kisayansi, kijamii, uchumi, imani na utamaduni katika jamii zetu kwa kiasi kama hiki ama zaidi ya hiki katika karne hii.