
BOOK OVERVIEW
Hadithi hizi ni matunda ya shindano la fasihi lililoshirikisha wanafunzi arobaini kutoka shule kumi za sekondari za wilaya ya Kisarawe na hadithi za washindi watatu zimetumika kufanya mkusanyiko na kutengeneza kitabu hiki. Hadithi zote zilibeba Kichwa cha habari kimoja ila ubunifu ndio umeleta tofauti toka hadithi moja mpaka nyingine, hata hivyo ili kunogesha utamu Walezi wa fasihi, wameamua kuzipa majina hadithi hizi ambapo zote awali zilikuwa na jina linalofanana mpaka nukta kwa kuwa ni zao la utunzi elekezi. TAFF iliamua kuendesha mashindano ya utunzi na baadae Tamasha la Fasihi ya Kiswahili ili kuwa jukwaa linaloshiriki sio tu kukuza maarifa ya jamii, bali pia kuwa sehemu ya kukabiliana na changamoto za kimaendeleo kwa kutumia Fasihi Andishi na Fasihi Simulizi.