Adili na Nduguze
Mchapishaji
Mbiu Press
Lugha
Swahili

Azima Kitabu Hiki

Expires on August 02, 2025

TSh 2,000/=

Chagua

MAELEZO YA KITABU

Adili na Nduguze ni hadithi fupi inayohusu maisha ya kawaida ya binadamu. Mwandishi wa kitabu hiki anajadili kwa kina dhana ya upendo kama kiini cha urafiki, mapatano, msamaha na wokovu dhidi ya madhila ya binadamu wenye moyo wa wivu, chuki na mabaya mengine yoyote.

Adili ni mhusika mkuu katika hadithi hii akiwa ni mtoto wa mwisho kuzaliwa katika watoto wa mzee Faraja, baba yao. Ndugu zake ni Hasidi na Mwivu. Kama lilivyo jina lake, Adili alikuwa adili kweli. Siku zote alitenda mema bila kujali changamoto zilizokuwepo. Alikuwa mwadilifu, mchapakazi, mwema, msamehevu na aliyetayari kujitesa kwa ajili ya wengine tofauti kabisa na kaka zake ambao walijawa na chuki na wivu.

Kutokana na uadilifu wake, Adili anapendwa na jamii nzima. Binadamu kupendwa na wanadamu wenzake ni jambo la kawaida lakini kupendwa na kuheshimiwa na viumbe wengine kama majini ni jambo lisilo la kawaida. Mfalme Rai  wa nchi ya ughaibu naAdili, liwaliwa Janibu walipendwa na kuheshimiwa na binadamu pamoja na majini

Ndugu zake adili kama jina la kitabu linavyosema “Adili na nduguze” walikuwa ni watu waliojawa na roho za chuki, wivu na tama kupita kiasi. Hawakupata kumpenda ndugu yao Adilina vilevile walikuwa wazembe katika kukilinda walichokipata. Wanamtosa baharini ndugu yao ili waweze kumuoa binti aliyeokolewa na Adili lakini binti mwenyewe anaamua naye kujitosa baharini ili tu asiolewe na yeyote kati yao wawili.

Katika kitabu hiki kimejaa mikasa mingi kama wahenga wanenavyo baada ya kisa mkasa. Mwandishi amakufunulia tijara ya wema “wema hauozi” ni msemo wenye hekima sana. Katika mkasa mmoja Adili anafanikiwa kumuokoa Huria binti kisasi, binti wa kijini ambaye baba yake kisasi alikuwa mfalme wa majini. Adili alipotoswa baharini, huria anakuja kumuokoa. Mjeledi mama yake huria anasema: “wema wako ulikuwa asilia, nawe ulitangulia kuutenda.” Adhabu ya ndugu zakeAdili kwa kumtupa baharini ilikuwa ni kugeuzwa manyani.

Je, ni kitu gani kilifuata baada ya ndugu zake adili kugeuzwa manyani? Adili, je aliishia wapi na wema wake? Nini kilimpata binti aliyejitosa baharini, je alikufa ama aliokoka? Fuatana na mwandishi huyu  hadi mwisho wa kisa hiki cha kusisimua.