BOOK OVERVIEW
Penzi la Harrison Urassa na mkewe Vannessa Williams lilikuwa motomoto. ilikuwa motomoto. Miaka minane ya ndoa yao ilikuwa yenye amani tele. Ni kama amekutana juzi tu!Afya ya Harrison au Harris kama alivyofupishiwa inakuwa chanzo cha tatizo jipya katika ndoa hiyo iliyokuwa imejaa amani na furaha tele.Harris akiwa jijini Mumbai, India kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji, anagundua mabadiliko makubwa kwa mkewe. Alihisi harufu ya kusalitiwa. Hakuwa akiwaza tofauti – ni kweli Vanessa alinasa kwenye penzi zito la kijana wa Kiarabu aliyeitwa Deus Ngoma. Kijana huyo akamchanganya na kumfanya Vanessa awe mtu wa
kujirusha na kumwacha mwanaye mchanga Junior akiwa na msichana wa kazi tu!
Kichaa cha mapenzi kilimpanda Vanessa na kujisahau kabisa kuwa mume wake angeweza kugundua mchezo mzima, tena kirahisi tu. Hapo ndipo ndoa inapogeuka chungu, huku machozi, majonzi na mateso yakichukua nafasi.Utumwa wa Mapenzi Nje ya Ndoa ni kazi nyingine nzuri ya JOSEPH SHALUWA ambapo hapa anakuthibitishia kuwa, hakujifunza kutunga bali alizaliwa akiwa na kipaji cha kubuni visa na kucheza na fasihi