Jambo la Maana
Mchapishaji
Mbiu Press
Lugha
Swahili
MAELEZO YA KITABU
Kitabu hiki ni matokeo ya tafsiri iliyofanywa na Ebrahim Hussein kutoka
katika kazi za mwandishi maarufu wa Kideni, Hans Christian Anderson.
Kitabu hiki kimebeba tafsiri za hadithi tatu: Nguo Mpya za Mfalme,
Jambo la Maana na Taa ya Zamani ya Barabarani. Kazi hii imejaa
mafunzo bora yanayoweza kuleta ukombozi wa kifikra na kuchagiza
mabadiliko chanya katika jamii.