
BOOK OVERVIEW
Anaitwa Janet Shelule. Mkasa wake ulianza siku
alipokutana na Rahimu. Rahim akamtongoza na
Janeth akamkubalia awe mpenzi wake. Mapenzi
yalikuwa mazuri licha ya kwamba Rahim hakuwa na
uwezo wa kutosha kifedha, biashara yake ya kuuza
matunda reja reja ilimnyima uwezo huo. Wakati huo
Janeth alikuwa akimalizia masomo yake ya kidato cha
nne. Alimpenda, Akampenda, wakapendana.
Shida ilianza pale marafiki zangu walipoanza kupata
simu za kisasa Smartphone kutoka kwa mabwana au
wazazi wao, huku yeye wazazi wake waki wa hawawezi
kumnunulia chochote. Ni hapo alipokumbushwa
asidharau dafu, embe tunda la msimu.
USIDHARAU DAFU, Embe tunda la msimu ni
hadithi iliyotolewa chini ya mradi wa Kitabu Kila Mahali
uliodhamria kurejesha ari ya usomaji wa vitabu nchini.
Mradi unaochapisha hadithi murua zilizo katika vitabu
vidogo vya bei nafuu ambavyo ni rahisi kusomwa na
kubebwa mahali popote.