
Kampa Kampa
Publisher
Lantern-E-Books
Language
Swahili
BOOK OVERVIEW
Aisha Kijavara, yule msichana mzuri mwenye urembo wa ulimbo alikuwa amejiinamia juu ya sofa zuri la thamani nyumbani kwa Babu Liwazo. Mbele yake kulikuwa wanaume wawili ambao hakuweza kuwatazama usoni kwa soni na majuto, usowe ulifurika machozi yaliyokuwa yakitoka bila kukoma katika kingo za macho yakeMacho yake makubwa na mazuri yalikuwa mekundu sana, kule kulia kwa muda mrefu kukiwa kumemfanya apoteze ile rangi yake ya asili. Rangi ya papai bivu. Mkononi alikuwa na kitambaa alichokuwa akitumia kujifutia machozi na mara kwa mara alikuwa akipandisha kamasi zilizokuwa zikikaidi kukaa zinapotakiwa kukaa. Naam, alijuta kumpa na kisha kumpa tena.