
BOOK OVERVIEW
Yawezekana ni kweli mvumilivu hula mbivu, lakini
kwa Rashida msemo huu haukuwa na maana.
Uvumilivu wake kwa mumewe umemfanya ale
zilizooza badala ya mbivu. Alikuwa anajua mumewe
Mwiya Ramadhani anampenda sana na ana wivu
kupindukia, lakini hakujua kama wivu wa mumewe
kwake ungekuwa mkali kiasi, kiasi cha kumfanya Rashida
ashindwe kumtazama yeyote usoni mpaka akafaikia
hatua ya kumwambia mumewe hunitii kiwewe. Wivu wa
Mwiya kwa mkewe ukoje? Fuatana na mtunzi wa mkasa
huu uone wivu wa kiwango cha lami.
Hunitii Kiwewe, …wewe ni kiwelewele ni hadithi
nzuri iliyotolewa chini ya mradi wa Kitabu Kila Mahali
uliodhamria kurejesha ari ya usomaji wa vitabu nchini.
Mradi unaochapisha hadithi murua zilizo katika vitabu
vidogo vya bei nafuu ambavyo ni rahisi kusomwa na
kubebwa mahali popote