Dakika ya Mwisho
Publisher
Lantern-E-Books
Language
Swahili
BOOK OVERVIEW
HIKI kilikuwa ni kikao kingine, miongoni mwa vikao vilivyofanywa na wanaume hawa watatu, ndani ya baa ya TGI Mtaa wa Ali Khan, Upanga jijini Dar es Salaam. Walipapenda hapo kwa kuwa palikuwa na utulivu mkubwa. Hapakuwa na wateja wengi, na hata hao waliofika walikuwa wastaarabu, wakizungumza kwa utulivu na kwa staha tofauti na baa za maeneo mengine.