Shujaa Mirambo
Publisher
Ape Network
Language
Swahili

Rent This Book

Expires on March 02, 2023

TSh 2,000/=

Choose Option

BOOK OVERVIEW

Tamthilia hii ya kihistoria inamhusu Mirambo, Mnyamwezi na mtemi wa Urambo toka mwaka 1860 hadi 1884. Mirambo alikuwa mwanajeshi na mtawala shupavu aliyetawala himaya kubwa upande wa magharibi ya Tanganyika. Kwa kutumia jeshi lake la vijana hatari waliojulikana kama Lugaluga [Rugaruga], Mirambo aliweza kulinda himaya yake na kuhakikisha kuwa anapokea ushuru stahiki kutoka kwa wafanyabiashara wa Kiarabu waliotoka Zanzibar na kufanya biashara ya watumwa, pembe za ndovu n.k. huko Kigoma, Kongo n.k. Wale waliokaidi amri ya mtemi waliishia kujifunza kwa majuto kuwa Mtemi Mirambo aliwazidi uwezo wa kivita na mamlaka ya utawala kwa kiwango kikubwa. Tamthilia hii ni kielelezo cha uzalendo na mwamko wa kisiasa wa hali ya juu wa Mtemi Mirambo mintarafu Mwafrika na uafrika wetu… Katika tamthilia hii, mwandishi anaibua visa na matukio kadha wa kadha ya kihistoria yanayobainisha ushujaa na uwezo mkubwa wa kivita na kiutawala wa mtemi huyu wa Kinyamwezi. Kutokana na uwezo wake mkubwa, mgeni kutoka Ulaya, H.M. Stanley, alishuhudia mikakati aliyokuwa anaitumia Mirambo vitani, alishangazwa sana na kukiri kuwa “Hakika Mirambo ni Napoleon Banaparte wa Afrika”.

COMMUNITY REVIEWS

There are no reviews for this book yet

Write a Review