
No video uploads for Emmanuel Mbogo |
Malkia Bibi Titi Mohammed
Tamthilia hii inamhusu Bibi Titi Mohamed, mwanamke aliyekuwa mstari wa mbele katika harakati za kudai uhuru wa Tanganyika. Kama mwanachama wa TANU na kiongozi wa Umoja wa Wanawake,
|
|
Nyerere na Safari ya Kanaani
Oktoba, 1966 kulizuka mgogoro mkubwa wa kihistoria kati ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Muhimbili.
|
|
Mtumwa Hadi Siti Binti Saad
Historia ya maisha ya Siti Binti Saad kama yalivyosawiriwa na Shaaban Robert na Nasra Mohamed Hilal, na sasa, katika tamthiliya hii ya kihistoria, itamfunulia msomaji wasifu na safari ya maisha ya mwanamama huyu.
|
|
Sadaka ya John Okello na Mapinduzi ya Zanzibar
Sadaka ya John Okello ni tamthilia ya kihistoria kuhusu mapinduzi ya tarehe 12/1/1964 visiwani Zanzibar.
|
|
Wangari Maathai
Mwaka 2004 Profesa Wangari Maathai, kiongozi wa chama cha kuhifadhi mazingira (Green Belt Movement) nchini Kenya, alitunukiwa tuzo ya Amani ya Nobel kutokana na mchango wake mkubwa katika harakati za kupigana amani, demokrasia, utawala bora, matumizi sahihi ya mazingira na rasilimali kwa manufaa ya kizazi hiki na vizazi vijayo kote ulimwenguni.
|
|
Tanzia ya Patrice Lumumba
KONGO [DRC] ilipata uhuru toka kwa Wabelgiji tarehe 30/06/1960 na Patrice Lumumba akawa Waziri Mkuu wa kwanza. Baada ya miezi sita tu, yaani tarehe 17/01/1961, Lumumba akauliwa kikatili na kinyama.
|
|
Fumo Liongo
Fumo Liongo alikuwa shujaa wa mji wa Pate katika Pwani ya Afrika ya Mashariki aliyeishi kati ya karne ya 9 na ya 13.
|
|
Siri za Maisha
Kama wewe ni mwanafunzi, mwalimu, mfanyabiashara, profesa, msanii, mkulima, fundi, mwanariadha au mama wa nyumbani, unao uwezo wa kubadilisha maisha yako katika nyanja yoyote ile kama unataka.
|
|
Watoto wa Maman’tilie
Katika riwaya hii ya Watoto wa Maman’tilie, mwandishi anathibitisha kuwa mama ni mtu wa muhimu sana. Riwaya inasimulia na kushadidia kuwa Maman’tilie ni nguzo na dereva wa familia yake yenye wasafiri watatu:
|
|
Nyerere na Vijiji Vya Ujamaa
Msingi na dafina ya tamthilia hii ni historia na lengo kuu la Mwalimu Julius Nyerere na TANU kutaka kujenga uchumi wa Ujamaa na Kujitegemea mintarafu mwongozo wa kitabu cha Azimio la Arusha, 1987.
|
|
Shujaa Mirambo
Tamthilia hii ya kihistoria inamhusu Mirambo, Mnyamwezi na mtemi wa Urambo toka mwaka 1860 hadi 1884. Mirambo alikuwa mwanajeshi na mtawala shupavu aliyetawala himaya kubwa upande wa magharibi ya Tanganyika. Kwa kutumia jeshi lake la vijana hatari waliojulikana kama Lugaluga [Rugaruga],
|
|
Mwinyi na Manyani ya Adili
Tamthilia hii inaangazia hali ya maisha nchini Tanzania kabla na wakati wa utawala wa Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi (Mhe). Tamthilia inaonesha Rais Mwinyi akipokea dola nchi ikiwa inaning’inia katika mtego mkubwa wa kifalsafa, kisiasa na kiuchumi, mtego uliowaweka wananchi katika lindi la taabu na ufukara usiomithilika.
|
|
Julius Nyerere Kizimbani
Tamthiliya hii inahusu tukio la kweli la kihistoria lililotokea mwaka 1958. Katika mwaka huo, TANU ikiwa na umri wa miaka minne pekee, serikali ya kikoloni ilidhamiria kuuyumbisha na hatimaye kuusambaratisha kabisa uongozi wa chama.
|
|
|
Morani
Tamthiliya ya Morani inasawiri misukosuko ya kisiasa na kiuchumi nchini Tanzania katika miaka ya 80. Katika kiwango cha uhalisia, tunamwona Dongo muhusika mkuu, akipambana na wahujumu uchumi....
|
|
Kumng'Oa Nduli
Tamthiliya hii inaakisi awamu mbili za utawala wa Dikteta Idi Amin nchini Uganda. Awamu ya kwanza ni kuanzia mwaka 1971 alipomng’oa Milton Obote na kujitangaza rais wa maisha wa nchi ya Uganda.
|
|
No award found
Ask Emmanuel Mbogo anything
No questions, Be the first to ask Emmanuel Mbogo
Contact Form