Fumo Liongo
Publisher
Ape Network
Language
Swahili

Rent This Book

Expires on March 02, 2023

TSh 3,000/=

Choose Option

BOOK OVERVIEW

Fumo Liongo alikuwa shujaa wa mji wa Pate katika Pwani ya Afrika ya Mashariki aliyeishi kati ya karne ya 9 na ya 13. Umaarufu wa Fumo Liongo ulitokana na ushujaa, uzalendo na kipaji chake cha umalenga miongoni mwa watu wa Pate na maeneo ya jirani. Kwa Mfalme Mringwari, ushujaa na umaarufu wa Liongo ni tishio kubwa dhidi ya utawala wake. Kilele cha hofu na chuki dhidi ya Fumo Liongo kinafikiwa pale Liongo anapoliongoza jeshi vitani na kuwashinda Wagala, maadui zao wa jadi. Licha ya kuitetea na kuilinda Pate dhidi ya wavamizi, Liongo hapati pongezi bali shukrani za punda kwani Mfalme Daudi Mringwari anapania aitoe roho yake. Anasema, “Nimelifuga joka hili tukutu ndani ya tundu la ufalme wangu … ila sasa nitaliteketeza kwa moto, niligeuze majivu baridi badala ya kulizika kiwiliwili.” Hakika ukianza kusoma hutaachia kitabu hiki hadi umejua mwisho wa kisa hiki cha kusisimua na cha kihistoria. Ni imani ya mwandishi na mchapishaji kuwa tamthilia hii itachochea fikra za wasomaji na kuzidi kutajirisha wapenzi ya lugha ya Kiswahili kwa vionjo na misamiati lukuki.

COMMUNITY REVIEWS

There are no reviews for this book yet

Write a Review