
BOOK OVERVIEW
Vigelegele, vifijo na cherekochereko za kina mama wakiimba mamie mwana so ukaule mgeni kengia ndizo zinazokamilisha kilele cha harusi ya Rahman, mtoto wa Alhaj Mwinyi Karim kwa Shufaa binti wa Mwinyi Sitaki Shari.
Hakuna kinachokosekana siku hiyo. Fahari yote na utajiri wa Alhaj Karim ulitengwa kukamilisha ndoa hiyo ili iwe harusi ya kusimuliwa. Ama kweli watu waliohudhuria walifurahi na kukubaliana kuwa, Rahman bin Mwinyi kapata; sio kama kakaye, Dakta Mustafa, ambaye hakua?ikiana na wazazi wake kwenye kuchagua mke.
Lakini ni kweli kwamba Rahman kapata mke “mtoto wa watu” au ni kama mkwezi mmoja kwenye karamu kubwa ya maulid ya harusi anavyojibu kwa dharau, “harusi za siku hizi harusi?”
Harusi si riwaya tu bali ni kielelezo cha mila na desturi za jamii ya watu wa mwambao wa pwani ya Afrika Mashariki. Ni wazi kuwa wasomaji wengi watafurahiwa na riwaya hii.