Sarafu ya Gavana
Mchapishaji
Wilbard Makene
Lugha
Swahili
MAELEZO YA KITABU
Watu wasiojulikana katika nchi ya Weusi Kusini, wanapambana vikali kumshambulia Gavana nchi hiyo, bwana Bongo kwa lengo la kummaliza. Katika hali ya kushangaza, vyombo vya usalama vya nchi ya Weusi Kusini, ambavyo vilipaswa kumpa ulinzi Gavana, vinasuasua kufanya hivyo. Hofu na mashaka vinatamalaki kichwani mwa Gavana; mnyororo wa maswali unajirefusha kichwani mwake.
Ndipo anapoibuka Elvis Madiba, kijana machachari toka ndani ya vyombo vya usalama. Anamfuata Gavana na kumwachia sarafu. Huo ndio unakuwa mwanzo wa kuibuka chuki na hasama, visasi na uhalifu, minyukano, nk