BOOK OVERVIEW
Tamaa ya kufika ng’ambo imeponza wengi. Wapo walioozea kifungoni, wapo waliokuwa chakula cha papa na wapo waliofanikiwa kufika ng’ambo lakini wanaishi na kulala mitaani na hawana namna yoyote ya kurudi nyumbani.
Usemi usemao Bongo bahati mbaya ni usemi wa kupigwa vita kila pande za nchi maana unadumaza uwezo wa kufikiri wa vijana wa Kitanzania wanaodhani maisha bora yanawezekana tu nchi za nga’mbo na si Tanzania. Ubunifu na kufanya kazi kwa bidii ndiyo njia pekee za kujiepusha, shida na umasikini na tamaa ya kutaka vitu vyepesi. Ni vyema kukubali kupokea changamoto na kuzifanyia kazi kupata matokeo tunayoyataka. Wepesi ama mwonekano wa wepesi usiwe kigezo cha maamuzi au egemeo la maisha yetu. Tusisahau usemi wa Kiswahili usemao Bahari shwari haitoi wanamaji stadi.
|
Amri Shaban
Vijana Jazz Band (Watunjatanjata ) - Waliimba Ngapulila ...fanya kazi kwa bidii utapata kaka, tamaa ya kufika ng´ambo imeponza wengi, wengine walijaribu..kuteka ndege nyara kwa kutumia silaha za bandia.............wahenga wananielewa. Kitabu hiki kimeeleza kwa kirefu ubaya wa tamaa ya kufika ngámbo bila kufuata utaratibu. |