Simu ya Kifo
                      
                                
                                
                                
                                
                                             Publisher 
                                        
                                        
                                            Ape Network
                                        
                                    
                                             Language 
                                        
                                        
                                            Swahili
                                        
                                    BOOK OVERVIEW
Mzee Jacob anafariki ghafla akiwa nyumbani kwake. Uchunguzi unabainisha kuwa amefariki kwa kuvuta sigara yenye sumu. Siku chache baadaye, bintiye, Mary anapigwa risai. Msururu wa vifo unaendelea kutokea mbali ya kuwa inspekta Wingo anajitahidi kufuatilia kwa karibu kuweza kubaini chanzo na mhusika wa mauaji haya. Mbaya zaidi, kila kifo kinapotokea, FAMBO anampigia inspekta Wingo simu na kumtaarifu kuwa punde si punde fulani atafariki.
Je, inspekta Wingo anaweza kutegua kitendawili na kuzuia kifo kinachotazamiwa kutokea? Na je, FAMBO ni nani hadi afahamu yajayo? Na je anahusika katika mauaji haya?










