Mbiu ya Mswahili
Publisher
Ape Network
Language
Swahili

BOOK OVERVIEW

Mbiu ya Mswahili ni bendera ya utamaduni inayopeperushwa na watu wa Afrika Mashariki walioko sehemu mbalimbali duniani. Dira ya kitabu hiki ni kutambulisha kazi za waandishi wa Kiswahili duniani kote. Kitabu hiki kina mkusanyiko wa mashairi yaliyoandikwa na waandishi wa Kiswahili wa tangu miaka ya 1940 hadi sasa. Pia kina maelezo mafupi ya vitabu zaidi ya 100 vya Kiswahili pamoja na taarifa za upatikanaji wake. Kitabu hiki kinapatikana duniani kote kupitia balozi za mataifa yanayotumia lugha ya Kiswahili na wadau wa Kiswahili walioko ughaibuni kama hidaya maalum kutoka kwa Waswahili kwenda kwa wageni na wapenzi wa Kiswahili. Kitabu hiki ni tunu ya utamaduni na utambulisho wa fasihi ya Kiswahili. Mbali na kuchapisha kitabu hiki, mradi wa Mbiu ya Mswahili pia unatoa machapisho maridadi ya tenzi na mashairi ya Kiswahili kwa ajili ya kuangika ukutani. Ni matumaini yetu kuwa kitabu hiki na vingine vitakavyofuata vitakuwa bendera itakayopepea kuonesha thamani na utajiri wa lugha aushi ya Kiswahili.

COMMUNITY REVIEWS

There are no reviews for this book yet

Write a Review