BOOK OVERVIEW
Kitabu hiki kimeandikwa kwa ustadi mkubwa ili kumwezesha mwanafunzi wa darasa la kwanza kusoma kwa ufasaha. Uandishi wa kitabu hiki umezingatia matakwa ya Muhtasari wa Elimu ya Msingi kwa Darasa la 1 wa Mwaka 2023. Matakwa hayo ni mwanafunzi kumudu stadi za awali za kusoma, zikiwamo: kutambua sauti za irabu na konsonanti, kutambua sauti za herufi mwambatano, kuunda silabi na maneno, na kutambua majina ya namba na majira ya saa. Kitabu hiki kimeandikwa kwa mpangilio mzuri, kina picha nyingi na hadithi za kuvutia. Haya yanamfanya mwanafunzi avutiwe na somo na awe na utayari wa kujifunza. Vilevile, kuna mazoezi na vitendo zaidi ya 100 pamoja na majaribio mwishoni mwa kitabu. Hivi vyote vinampa mwanafunzi fursa sahihi ya kutendea kazi kile alichofundishwa na mwalimu, hivyo kuweza kujenga umahiri unaotakiwa. Tunaamini kuwa kitabu hiki kikitumika shuleni, kila mwanafunzi atakuwa mahiri katika stadi za kusoma. Matokeo yake, atafurahia si tu somo la Kiswahili bali pia masomo mengine kwa vile atasoma kwa urahisi na kwa mtiririko sahihi wa mawazo. APE Networ