BOOK OVERVIEW
Kitabu hiki kimeandikwa kwa kuzingatia matakwa ya Muhtasari wa Elimu ya Msingi kwa Darasa la 1 wa Mwaka 2023. Matakwa hayo ni kumjengea mwanafunzi umahiri katika uumbaji wa herufi, uandishi wa maneno, uandishi wa sentensi fupi, utumiaji wa alama za uandishi na uandishi wa habari fupi. Kitabu kimepangwa vizuri na kina picha nyingi za kuvutia. Vilevile, kina mazoezi 137 pamoja na majaribio mwishoni mwa kitabu. Hivi vyote vinampa mwanafunzi fursa sahihi ya kufanyia kazi kile alichojifunza katika mchakato wa ujifunzaji ili kujenga umahiri unaotakiwa. Tunaamini kuwa kitabu hiki kikitumika, mwanafunzi atakuwa mahiri katika stadi za kuandika. Matokeo yake yatamfanya afurahie si tu somo la Kiswahili bali pia masomo mengine kwa kuwa ataandika kwa mwandiko unaosomeka kwa urahisi.