Kaptula la Marx
Publisher
Ape Network
Language
Swahili

Rent This Book

Expires on March 02, 2023

TSh 4,000/=

Choose Option

BOOK OVERVIEW

Tamthiliya ina sehemu 6 ambako mchezo hubadilisha mahali pake kati ya gereza lenye wafungwa 6 pamoja na kiongozi wao "Mwangaza Africanus" na serikali ya nchi isiyotajwa jina chini ya raisi anayeitwa Kapera.

Chanzo ni jaribio la wafungwa gerezani kukusanya habari nyingi za "dunia ya nje" iwezekanavyo kwa kuiangalia kupitia shimo dogo ukutani.

Wakati huohuo raisi anayeitwa Kapera baada ya kusoma Marx anaamua kubadilisha siasa yake kwa manufaa ya watu wengi. Kwa kusudi hii anaamua kuvaa "kaptula la Marx" na shati ya Mao. Nguo zote mbili ni kubwa mno kwake. Mawaziri wake wanamwitikia na kuvaa vilevile. Pamoja wanaondoka walipo kutafuta nchi ya usawa. Katika sehemu ya 4 wanaondoka kuelekea nchi ya usawa na undugu. Njiani wanakutana na jitu anayeitwa "Korchnoi Brown" na kuwapa maelekezo. Lakini wanashindwa kufika kwa sababu mawaziri hawafai.

Wafungwa gerezani wakati huohuo wanafanya maigizo kati yao wakijadili siasa ya nchi. Mwangaza Africanus anasoma ujumbe kwa viongozi wa Afrika anapokataa siasa zao.

Mawaziri wanaonyeshwa baadaye jinsi walivyo kama vipofu na kutumia mateso ya wafungwa kama mbinu.

COMMUNITY REVIEWS

There are no reviews for this book yet

Write a Review