BOOK OVERVIEW
Kitabu hiki kimeandikwa kwa kuzingatia Muhtasari wa somo la Historia ya Tanzania na Maadili kwa darasa la tatu wa shule za msingi Tanzania wa mwaka 2023. Uandishi wake umezingatia malengo ya elimu Tanzania, malengo ya elimu ya msingi na umahiri wanaopaswa kupata wanafunzi baada ya kujifunza somo hili. Kwa sababu hiyo, kitabu hiki kina picha na michoro ya kutosha kumsaidia mwanafunzi kuelewa kwa urahisi. Pia, kuna kazi za kufanya zinazolenga kumsaidia mwanafunzi kukuza ujuzi wa kuwasiliana, kushirikiana, kujenga fikra tunduizi, kufanya maamuzi na kujenga tabia ya kujifunza bila kukoma. Kitabu kimepangwa katika sura tisa: Historia ya Tanzania; urithi wa Tanzania; Maadili ya Taifa; Wajibu na haki za mtoto; Kuheshimu na kutii sheria; Maarifa na ujuzi wa asili wa jamii; Ushirikiano na uhusiano baina ya jamii za Kitanzania; Uongozi katika familia na ukoo; na Uongozi shuleni. Vilevile, kitabu kina mazoezi ya kutosha kumsaidia mwalimu au mzazi kumpima mtoto; au mwanafunzi kujipima mwenyewe ili aone kama ameweza kupata maarifa na ujuzi uliokusudiwa katika mada husika.