
EUPHRASE KEZILAHABI SEHEMU YA KWANZAFlorida Kezilahabi mke wa Euphrase Kezilahabi akitoa historia ya mume wake kabla ya kuwa mtunzi wa vitabu.
|
|
EUPHRASE KEZILAHABI SEHEMU YA PILIFlorida Kezilahabi mke wa Euphrase Kezilahabi akitoa historia ya mume wake, safari zake pamoja na utunzi wake n.k
|
|
Gamba la Nyoka
Gamba la Nyoka ni riwaya inayoonyesha jinsi maamuzi ya kisiasa yasiyotafakariwa yanavyoweza kuwa na athari mbaya kwa wanyonge na wakulima.
|
|
Kichwamaji
Riwaya ya Kichwa Maji ni Riwaya iliyoandikwa mwaka 1974 na E. Kezilahabi. Hii ni Riwaya ya Kisaikolojia kwa sababu inadodosa nafsi ya mhusika, fikra, hisia, mawazo, imani, hofu, mashaka, matumaini na matamanio yake binafsi na athari za mambo hayo kwake na kwa jamii yake.
|
|
Kaptula la Marx
Chanzo ni jaribio la wafungwa gerezani kukusanya habari nyingi za "dunia ya nje" iwezekanavyo kwa kuiangalia kupitia shimo dogo ukutani.
|
|
Dunia Uwanja wa Fujo
“Dunia uwanja wa fujo” inaelezea jinsi maisha yaliyopo duniani ni sawa sawa na fujo kwani kila mtu anayekuja duniani huleta fujo zake na baadae kutoweka.
|
|
Nagona
Nagona ni riwaya fupi ya kifalsafa na kibaadausasa inayoibua fikra juu ya falsafa na maana ya uhai, maisha, dhamiri na hata fikra yenyewe. Mhusika kiini wa novela hii anajikuta katika mazingira ya ajabuajabu katika nyakati tofauti tofauti.
|
|
Mzingile
Mzingile ni novela (riwaya fupi) ya kifalsafa na kibaadausasa iliyochapishwa kwa mara ya kwanza mwaka 1991. Riwaya hii ni pacha ya ile ya Nagona (1990). Riwaya hii inasawiri chimbuko, maendeleo, maangamizi na kuzaliwa upya kwa dunia kutokana na fujo za wanadamu.
|
|
Dhifa
Dhifa ni diwani ya mwisho ya Kezilahabi. Diwani hii inakusanya tungo za miaka ya 1990-2008, wakati wa mageuzi ya kiliberali mamboleo yaliyoasisiwa na Rais Ali Hassan Mwinyi na kuendelezwa na warithi wake baada ya Mwalimu J.K. Nyerere kustaafu.
|
|
Karibu Ndani
Karibu ndani ni diwani ya pili ya Kezilahabi. Hii imekusanya mashairi yaliyohusu harakati za Ujamaa nchini Tanzania, hususani “kushindwa” kwa Ujamaa kutokana na unjozi na upofu wa waasisi wake; mgogoro wa ushairi wa miaka ya 1970 kati ya wanajadi na wanamabadiliko, tafakuri kuhusu maisha ya kawaida, na kuhusu falsafa
|
|
Rosa Mistika
Rosa Mistika ni riwaya inayohusu masaibu ya msichana Rosa aliyelelewa katika mazingira ya udhibiti wa kidini na kimila katikati ya lindi la umaskini; na baadaye akakabiliwa na vishawishi pale alipoingia katika shule ya bweni na kisha chuo cha ualimu.
|
|
Kichomi
Kichomi ni diwani inayoakisi mawazo anuwai kutoka kwenye nyanja tofauti za maisha, kama vile uchumi, siasa, utamaduni, ndoa na dini; hususan katika sehemu ya kwanza ya diwani aliyoiita Mashairi ya Mwanzo.
|
|
No award found
Ask Euphrase Kezilahabi anything
No questions, Be the first to ask Euphrase Kezilahabi
Contact Form