
Zawadi ya Wino
Mchapishaji
Gloria D. Gonsalves and Eric F. Ndumbaro
Lugha
Swahili
MAELEZO YA KITABU
Kitabu hiki kina nia moja kuu: Kumfanya mtoto apende kusoma vitabu. Lakini kabla ya kufanikisha hilo, inabidi tumueleweshe mtoto wetu kwanza kwa nini vitabu ni muhimu katika maisha yake.
Tumemwandikia mtoto wetu barua zenye mifano mbalimbali kuhusu umuhimu na uhondo wa vitabu. Tunatumaini kuwa barua hizi zitampa kiu ya kutaka kuthibitisha yaliyoandikwa humo.
Basi wewe mzazi, mwalimu na mlezi, jipatie kitabu hiki kama unataka kumpa nafasi mtoto wa jamii yetu kujenga tabia ya usomaji vitabu akiwa shuleni, nyumbani au popote.