Kiswahili Kwanza Kidato cha Tano & Sita na Elimu ya Juu
Publisher
Ape Network
Language
Swahili

Rent This Book

Expires on August 02, 2025

TSh 3,000/=

Choose Option

BOOK OVERVIEW

“Maarifa yoyote ya mtu yanakuwa na mantiki pale yanapoweza kuwafikia watu wengi zaidi ambao watayatumia katika kutanzua mikwamo yao ya taaluma na maisha kwa ujumla”. Kiswahili-1: Nadharia ya Lugha Kidato cha Tano, Sita na Elimu ya Juu nikitabu kilichoandikwa kwa kuzingatia Muhtasari wa Kiswahili Kidato cha Tano na Sita ambao ulianza kutumika mwaka 2010. Sanjari na kuwahusu wadau wa kidato cha Tano na Sita, yaani wanafunzi na walimu, kitabu hiki pia kitawafaa sana wanafunzi wa Stashahada (Diploma) na wanafunzi wa shahada ya kwanza katika vyuo vikuu, hususani kwenye mada za Historia ya Kiswahili, Semantiki, Tafsiri na Ukalimani. Aidha, Kiswahili-1: Nadharia ya Lugha Kidato cha Tano, Sita na Elimu ya Juu kimeandikwa kwa kuzingatia mabadiliko yanayotokea katika nyanja za siasa, uchumi, sayansi, teknolojia, utamaduni na elimu. Kitabu hiki kimeenda sambamba na kukua na kuenea kwa matumizi ya Kiswahili katika nchi za Afrika Mashariki, Afrika na nje ya Bara la Afrika, kama vile Ulaya, Marekani na Asia. Kitabu kina mada zote zinazotakiwa kufundishwa katika Kidato cha Tano na Sita na kimejikita katika mkabala wa sasa wa mbinu shirikishi za kujifunza na kufundishia ambazo ufundishaji na ujifunzaji umemlenga zaidi mwanafunzi kwa kumjengea ujuzi na utendaji. Kiswahili-1: Nadharia ya Lugha Kidato cha Tano, Sita na Elimu ya Juu kimegawanyika katika sura sita, Kila sura imefafanuliwa kwa kina. Sura za kitabu hiki zimepangwa kama ifuatavyo: Sura ya Kwanza yenye mada ya Maendeleo ya Kiswahili imejikita katika kujadili Asili ya Kiswahili kwa kubainisha na kufafanua kwa kina nadharia mbalimbali za Asili ya Kiswahili na Chimbuko la Kiswahili. Pia, suala la Usanifishaji wa Kiswahili limejadiliwa kwa kina katika sura hii. Aidha, maelezo yametolewa kuhusu kukua na kuenea kwa Kiswahili kabla na baada ya Uhuru hadi sasa nchini Tanzania, Kenya na Uganda. Sanjari na hayo, suala la kukua na kuenea kwa Kiswahili katika nchi za Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kabla na baada ya uhuru hadi sasa limejadiliwa. Vilevile, kuna maelezo kuhusu Chama cha Kiswahili cha Afrika Mashariki (CHAKAMA) na Chama cha Wanafunzi wa Kiswahili wa Vyuo Vikuu Afrika Mashariki (CHAWAKAMA). Mbali na hayo, maelezo kuhusu juhudi za kukuza, kueneza na kuendeleza matumizi ya Kiswahili katika nchi za Umoja wa Afrika pamoja na juhudi za kukuza, kueneza na kuendeleza matumizi ya Kiswahili nje ya Afrika yamejadiliwa kwa kina. Sura ya Pili inahusu Matumizi ya Sarufi. Katika mada hii, vipengele muhimu vinne, ambavyo ni Fonolojia, Mofolojia, Sintaksia na Semantiki vimejadiliwa kwa kina. Kipengele cha Fonolojia kimefafanua kuhusu matamshi, kiimbo, mkazo, lafudhi, otografia na dhana ya Fonetiki kwa ufupi. Kipengele cha Mofolojia kimefafanua kuhusu mofimu, uambishaji, mnyambuliko na aina saba za maneno. Aidha, kipengele cha Mofolojia kimejumuisha suala la Ngeli za Kiswahili, Matumizi ya O-rejeshi na Makosa ya Kisarufi na Kimantiki. Kipengele cha Sintaksia kimefafanua kuhusu dhana ya Sintaksia kwa kulenga zaidi tungo neno, kirai, kishazi na sentensi. Pamoja na hayo, suala la muundo wa sentensi na uchanganuzi wa sentensi kimapokeo na kimuundo ni mambo ambayo yamejadiliwa kwa kina katika kipengele cha Sintaksia. Aidha, katika kipengele cha Semantiki, mjadala umejikita kwenye maana katika neno na katika sentensi; maana ya maana ambapo nadharia nne za maana zimebainishwa na kufafanuliwa kwa kina; pamoja na aina za maana katika lugha.

COMMUNITY REVIEWS

There are no reviews for this book yet

Write a Review