BOOK OVERVIEW
Jamii ya sasa imekuwa na mtazamo tofauti sana kuhusiana na mafanikio. Wengi wanadhani kuwa na mali, vitu na pesa ndio mafanikio ya kweli. Wapo waliovipata vyote hivi lakini ndani yao bado wakabaki na ombwe “vacuum/ emptiness” wakihitaji utoshelevu mwingine wa zaidi. Hii inatupa ukweli kwamba mafanikio ya kweli ya kila mwanadamu nipale anapoweza kuwa vema kiroho, kiakili, kijamii (kuwa na mahusiano mazuri na wanaomzunguka), kisaikolojia (ubora wa nafsi na tabia), kimwili (uzima wa afya) na kiuchumi pia. Eneo lolote kati ya haya likiyumba, ujumla wako wote unakuwa haujakaa sawa “you become unbalanced”. Kwa kuzingatia na kuyaweka kwenye matendo yote yaliyoko kwenye kitabu hiki utaweza kupenya hatua kwa hatua kuelekea kwenye mafanikio yako ya kweli. Wengi wamesaidika na mafundisho haya kupitia Televisheni, vipindi vya redio na makongamano. Sasa wewe unapata fursa ya kuyasoma mafundisho haya katika mjumuisho. Chukua nafasi hii kuyabadilisha maisha yako mwenyewe. Wakati ni huu. Nakutakia kuyafurahia mafundisho haya.