
BOOK OVERVIEW
Jifunze Lugha ya Kiswahili ni kitabu kinacholenga kutoa mwongozo kwa wanafunzi na wageni wanaojifunza lugha ya Kiswahili kwa hatua ya awali. Kitabu hiki, ni msaada mkubwa kwa wanagenzi wa lugha ya Kiswahili kwani kimetumia mbinu rahisi ambazo zitamsaidia mwanafunzi kujifunza hata akiwa mwenyewe. Kitabu kimetumia picha na mifano rahisi yenye uhalisia kwa kiasi kikubwa katika mazingira yanayotuzunguka. Lugha iliyotumika ni lugha nyepesi na rahisi kwa mtumiaji hasa yule anayejifunza lugha ya Kiswahili kwa mara ya kwanza. Jambo jema zaidi kuhusu kitabu hiki ni kwamba, si msaada kwa wanaojifunza tu pekee bali kitawasaidia hata wale wajuzi wa lugha ya Kiswahili katika kuongeza maarifa. Nawakaribisha wote tusome kitabu hiki kuanzia mwanzo hadi mwisho.