
Fundi Hakatai Tenda
Publisher
Lantern-E-Books
Language
Swahili
BOOK OVERVIEW
Fred Babilo alikuwa kijana mzuri mwenye matarajio na malengo makubwa kabisa. Shida ilianza pale alipoanza kupata mafanikio na kuyatumia vibaya, starehe zikiwa kipaumbele chake namba moja hata akajikuta akitembea na kila msichana mzuri aliyemuona.Fedha zake zikiwa ulimbo, aliwapata wengi kwa kadiri alivyoweza. Na katika hilo alivunja ndoa za watu wengi, kuharibu malengo ya wanafunzi kwa kuwapa ujauzito na mengine mengi mabaya. Wengi walilizwa na kuumizwa naye na kwa kuwa alikuwa na fedha na wakati ule utawala wa kuheshimu sheria ukiwa jina, hakuna aliyeweza kumfanya chochote. Akasahau kazi ya fundi huwa ni kupokea tenda na sio kuzikataa. Kilichomkuta hakisimuliki.